Mavazi ya usiku kwa mtu mnene na mwembamba

Mavazi ya usiku kwa mtu mnene na mwembamba

Haya haya kumekucha wajameni, sasa leo katika fashion tumekujia na jambo konki kabisa. Tutaangalia kuhusiana na mavazi mazuri ambayo yatakupendeza na kuonekana wa tofauti ukumbini na sio mavazi tu, hadi rangi ambazo zinakuwa na muonekano mzuri usiku.

Cha kuzingatia ni kuangalia mwili wako utapendeza vazi gani. Kama wewe ni mtu mnene, tafuta nguo ambayo haitokubana sana na kukuonesha maumbile yako na kama wewe ni mwembamba, vaa nguo ambayo inaendana na mwili wako, ikiwezekana kabla hujatoka uliza mtu wa karibu yako kuwa unaonekanaje ndo uweze kutoka ili kuepuka kuwa kichekesho katika shughuli za watu.

Wanawake wengi wakialikwa kwenye shughuli ya aina yoyote ile anatamani apendeze kuliko mtu yoyote yule, hivyo basi kama unahitaji kupendeza, basi inabidi utumie gharama kubwa kweli kweli, kama wasemavyo waswahili, raha ya uzuri uzurike, sasa hapa utazurika kwa kutoa gharama kubwa.

Aina ya rangi zinazopendeza kwa nguo za usiku

Rangi ya gold au dhahabu

Rangi ya dhahabu inakupa kujiamini na kukupatia muonekano ambao kila mtu atakuwa anakutazama wewe kwa sababu rangi hiyo wakati wa jioni inaonekana vizuri kuliko ukivaa asubuhi au mchana.

Rangi ya maroon au nyekundu

Hizi ni rangi ambazo watu wanazichukulia kawaida sana ila ndo zinaleta muonekano mzuri ukiwa ukumbini. Usiku zinakupatia muonekano wa tofauti kabisa, so rangi nyingine ambayo ntakushauri utumie kwa ajili ya mtoko au shughuli ya usiku ni maroon na velvet nyekundu.

 

Rangi ya zambarau

Zambarau ni rangi ambayo inampa mtu hadhi fulani ukiwa unachagua nguo na rangi ya kwendea kwenye shughuli za usiku, nakushauri rangi hii kwasababu inakupa muonekano mzuri na kukugeuza kuwa kama malaika.

Rangi nyeusi na nyeupe


Hizi ni rangi ambazo ni vipenzi vya watu wengi, rangi itakayo kupatia muonekano wa kuvutia zaidi. Siku hizi watu wengi wanapenda sana rangi ya off white na nyeusi ya kukoza, rangi hizi kwanza zitakufanya ujiamini sana maana hakuna mtu anayepinga katika rangi nyeusi au nyeupe.

Nguo yenye lace
Lace ni nguo ambayo inapendwa na kila mtu. Ukiona tu hata kwa mara moja lazima ikuvutie, so ukiwa unachagua nguo ya kwenda kwenye shughuli, ukiona nguo yenye lace usiizarau maana ikivaliwa na mtu yoyote yule awe mwembamba au mnene inampatia muonekano mzuri mno na wakati mwingine unaweza kumpita hadi bibi harusi mwenyewe.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post