Aliyetamba na wimbo wa Jambo Bwana afariki dunia

Aliyetamba na wimbo wa Jambo Bwana afariki dunia

Mwanamuziki wa Kenya Teddy Kalanda Harrison ambaye alipata umaarufu kupitia wimbo wa ‘Hakuna matata/Jambo bwana’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72.

Taarifa ya kifo chake imetolewa na mdogo wake John Katana kwa kueleza kuwa Kalanda ambaye alikuwa mwanzilishi wa bendi ya Them Mushrooms alifariki jana Septemba 17, nyumbani kwake Kaloleni, Kaunti ya Kilifi baada ya kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu.

Utakumbuka kuwa mwanamuziki huyo aliweka wazi kusumbuliwa na ugonjwa huo katika mitandao ya kijamii mwaka 2018.

Bendi ya Them Mushrooms ilianzishwa mwaka 1969 na ndugu pamoja na marafiki wa karibu wa Teddy wakiwemo Billy Sarro, George Zirro, Pius Plato Chitianda, John Katana, na Pritt Nyale.

Enzi za uhai wake Teddy alishirikiana na wenzake katika bendi hiyo kutoa ngoma mbalimbali ikiwemo iliyowafanya watambulike zaidi ya ‘Jambo bwana’, Unkula Huu, Wazee Wakatike, Nyambura, Ndogo Ndogo, Hapo Kale na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags