Tuzo za Mimi Mars zipo huku, sio huko!

Tuzo za Mimi Mars zipo huku, sio huko!

Ni miongoni mwa mastaa Bongo waliojaliwa vipaji vingi, hakuna ubishi kuwa Mimi Mars amefanikiwa kutengeneza jina lake katika muziki na filamu kitu kinachomfanya kuwa chapa yenye uwawishi katika tasnia.

Miaka yake saba katika Bongofleva ameshirikiana na wasanii kama Nandy, Marioo, Young Lunya, Nikki wa Pili, Mwana FA, Abigail Chams, Kagwe Mungai, AY, Quick Rocka, Dogo Janja, Darassa n.k. Huyu ndiye Mimi Mars.

Akiwa na umri wa miaka 11 tu, tayari sura ya Mimi Mars ilishasambaa katika vituo vya runinga baada ya kucheza tangazo la moja ya kampuni za kuuza magodoro nchini na alifanya vizuri na ni kitu anachojivunia hadi sasa.



Tangu akiwa mdogo alipenda muziki na miongoni mwa wasanii waliomvutia ni Usher Raymond IV, mshindi wa tuzo za Grammy mara nane aliyepata umaarufu mwishoni mwa miaka ya 1990 kufuatia kuachia albamu yake ya pili, My Way (1997).

Kabla ya muziki, Mimi Mars alianza kutangaza katika runinga akiwa na kipindi chake cha umbea, Weekend Gossip kupitia TV1, na baada ya kutoka kimuziki akaonekana tena kwenye kipindi cha The Trendy Show akiwa na Cynthia Mziray na Anita Mwiru.

Baada ya kusainiwa na rekodi lebo ya dada yake, Mdee Music, wimbo wa kwanza wa Mimi Mars kuutoa, Sugar (2017) ulitengenezwa studio kwa Barnaba, High Table Sound ambayo imetengeneza nyimbo nyingi za Barbana. Kufanya vizuri kwa wimbo huo, kulipelekea Coke Studio Africa kumpa Mimi Mars nafasi ya kutumbuiza kama Msanii Chupukizi (Big Break Artist) 2018 akitabiriwa kuja kufanya makubwa katika muziki.



Hadi sasa akiwa ametoa EP mbili, The Road (2018) na Christmas with Mimi Mars (2021), bado hajashinda tuzo yoyote katika muziki wake ingawa upande wa filamu ameshinda tuzo mbili kutoka Tanzania Film Festival Awards 2021 na The Orange Awards 2022.

Muigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael ambaye amechukua nafasi ya Mimi Mars (Maria) katika tamthilia ya Jua Kali, ni miongoni mwa waigizaji ambao Mars aliwahi kuwafuata hapo awali akiwaomba wampe fursa katika tasnia ila hakufanikiwa kwa wakati huo.

Hadi dada yake, Vanessa Mdee anatangaza kuachana na muziki, Mimi Mars alikuwa hajarekodi naye wimbo wowote wa Bongofleva zaidi ya wawili hao kushirikishwa na dada yao mkubwa, Nancy Hebron katika wimbo wake wa Injili, Beautiful Jesus (2017).

Mimi Mars ni miongoni mwa waliomfundisha Marioo lugha ya Kiingereza aliyeishia kidato cha pili, pia huyu ndiye msanii wa kike Bongo aliyemshirikisha zaidi Marioo wakiwa wametoa nyimbo mbili pamoja - Una (2019) na La La (2022). Hiyo ni sawa na Wema Sepetu ambaye alimfundisha Diamond Platnumz lugha ya Kiingereza. Na Wema, Miss Tanzania 2006 ndiye mrembo Bongo aliyetajwa zaidi kwenye ngoma za Diamond zikiwemo Nimpende Nani (2012), Kesho (2012), Fire (2017) na kadhalika.



Mwana FA na AY ndio wasanii pekee Bongo waliofanya kazi na Vanessa Mdee na Mimi Mars ambao ni ndugu. Mimi Mars kamshirikisha Mwana FA katika wimbo Ex Remix (2019), huku Mwana FA akimshirikisha Vanessa katika wimbo Dume Suruali (2016).

Kabla ya Whozu kuwa na Tunda aliyetokea kwenye video ya wimbo wake Doko (2019), kisha Wema Sepetu ambaye pia kamtumia katika video yake Ameyatimba (2023), staa wa mwanzo kutamani kuwa naye kimahusiano alikuwa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags