Makabila Azungumza Kuhusu Mwonekano Wake Mpya

Makabila Azungumza Kuhusu Mwonekano Wake Mpya

Msanii wa singeli, Dulla Makabila wiki hii 'ametrend' baada ya kutupia picha yenye mwonekano mpya ikimuonesha kung'aa zaidi sura na kuwa mweupe.

Kutokana na mwonekano huo, baadhi ya mashabiki wake wameonekana kuhoji kupitia mitandao ya kijamii wakidai huenda msanii huyo akawa anatumia vipodozi vikali.

Mwananchi imemtafuta Dulla na kupiga nae story kuhusu tuhuma hizo,

Mwananchi: Naona unamwonekano mpya, una kipara kama Billinas na uso umekuwa mweupe, nini siri ya huo weupe?

Dulla Makabila: Hili ndiyo unataka kuniuliza nakujua dada yangu (kicheko) ila wewe bana, haya najichubua natumia mkorogo wa gharama sana.

Mwananchi: Nini hasa kilisababisha ufanye hivyo ikiwa wewe ni mtoto wa kiume?

Dulla Makabila: Ni mapito tu ya ujana. Unajua unapokuwa katika hatua hiyo unahitaji kujaribu kila kitu na napenda kuwa mweupe hakuna kitu kingine, japo mimi ni mweupe.

Mwananchi: Lakini unaona michambo ya ‘comment’ kuhusu mwonekano wako huo wa kuwa mweupe?

Dulla Makabila: Naona na nasoma, mashabiki zangu wapunguze hasira mimi sijaua jamani, waache kumshambulia kwani haya ni mapito.

Mwanaspoti: Na upara imekuwaje tena ama umeamua kumuiga Billinas?

Dulla Makabila: (Kicheko) Hapana bana, hii nilikuwa nafanya video ndiyo maana nikanyoa na ndiyo basi tena nitakuwa na huu muonekano sirudi tena kwenye nywele na Billinas aliponiona alinipongeza kuwa na kipara, kiufupi amependezewa mimi kuwa kama yeye kichwani.

Mwananchi: Muziki wa Singeli kwa sasa unabamba sana na tunaona wasanii wengi wanahamia huko akiwemo Diamond, Jux, Harmonize la, Ally Kiba na wengine wengi, wewe binafsi umejipangaje kwao na je unaonaje, wamewezea?

Dulla Makabila: Singeli ina nafasi kubwa sana kwani ukiangalia hata kwenye matamasha ya serikali inapigwa, msanii wa Bongo Fleva anaweza kulipwa pesa nyingi huku msanii wa Singeli akalipwa kidogo lakini bado wa Singeli akateka mashabiki kuliko wengine.

Ila mie niwaambie tu kaka zangu wajipange haswa wasidhani huku kwenye Singeli wataweza kutukimbiza, huku niko mimi Mfalme wa Singeli ambaye nimeshindikana kushushwa cheo changu, na niseme tu wamejitahidi kuimba Singeli ila hawataweza kunifikia mimi.

Mwananchi:Tutegemee ndoa lini tena?
Dulla Makabila: Jamani kila wakati nitakuwa naoa mimi tu, ndoa mbili nimeona zimenishinda unataka nioe tena? Subiri kwanza kidogo nipo kwenye kuchagua mtu sahihi.

Mwananchi: Kwani uliowaoa mwanzo hawakuwa sahihi?
Dulla Makabila: Sitaki usinitafutie matatizo na wanawake (kicheko) kwanza nina mchumba tayari.

Mwananchi: Hivi unapokuwa na hasira cha kwanza unafanya nini?
Dulla Makabila: Mara nyingi napenda kuondoka eneo la tukio ili kuepusha shari.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags