Je Wajua, Mshahara Ulikuwa Unaitwa Pesa Ya Chumvi

Je Wajua, Mshahara Ulikuwa Unaitwa Pesa Ya Chumvi

Kila ifikapo mwisho wa mwezi wafanyakazi kutoka mashirika mbalimbali akili yao huwa ni moja tuu kupokea mshahara ili aende kumwagilia moyo, lakini wengi wao hawaju maana ya neno ‘Mshahara’ ambapo zamani neno hilo lilikuwa likiitwa ‘Pesa ya Chumvi’.

Dhana ya mshahara imekuwa na sura tofauti kabla ya kuwa kile tunachokifahamu leo kama malipo ya fedha kwa kazi iliyofanyika.

Kwa mujibu wa wanahistoria wa lugha, asili ya neno ‘Mshahara’ linauhusiano wa moja kwa moja na neno la Kiarabu ‘Ajra’ likiwa na maana ya malipo au ujira.

Aidha kabla ya mfumo wa kutumia pesa kununulia vitu, wafanyakazi walikuwa wakilipwa bidhaa kama vile chumvi, nafaka au mavazi, ambapo Roma ya kale askari walikuwa wakipewa malipo kwa njia ya chumvi ndipo neno la Kingeereza ‘Salary’ lilipozaliwa kutokana na neno la Kilatini ‘Salarium’ likiwa na maana ‘Malipo/Pesa ya Chumvi’.

Kati ya karne 3 K.K. hadi karne ya 1 B.K waajiri walikuwa wakitumia neno hilo kutokana na chumvi kuwa ndio bidhaa adimu na yenye thamani kwa kipindi hicho.

Kwa upande wa Kiswahili, wataalamu wa lugha wanaeleza kuwa neno "mshahara" lilianza kutumika rasmi wakati wa ukoloni, likiwa na maana ya ujira wa mkataba au ajira ya serikali, hususani kwa waajiriwa wanaolipwa kila mwezi.

Mbali na hayo yote kwa sasa neno hilo limekuwa likipata misamiati mipya mfano ‘Maokoto’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags