Ngoma ngumu kwa Diddy, vilainishi nyumbani kwake vyageuka gumzo

Ngoma ngumu kwa Diddy, vilainishi nyumbani kwake vyageuka gumzo

Ikiwa ni siku moja imepita tangu mwanamuziki wa hip-hop Marekani Sean 'Diddy' Combs kutiwa nguvuni, ripoti mpya ya kilichokutwa kwenye nyumba zake yatolewa.

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka wa Diddy wamesema wakati nyumba za mkali huyo zilizopo Los Angeles na Miami zilipofanyiwa upekuzi na Maafisa Usalama mwezi Machi mwaka huu, ndani kulikutwa na vitu kama vile dawa za kulevya zaidi ya chupa 1,000 za mafuta ya watoto na vilainishi.

Mbali na hayo, utakumbuka awali baada ya msako zilitolewa taarifa ya kuwa ndani kumefungwa kamera za siri.

Ikumbukwe mkali huyo alikamatwa jana Jumanne Septemba 17, 2024 na kutupwa mahabusu, kwa taarifa zilizopo sasa amenyimwa dhamana na Jaji wa Mahakama ya Shirikisho ya Lower Manhattan, hivyo amepelekwa kwenye gereza ambalo msanii mwenzie R. Kelly ndipo anatumikia kifungo chake.

Kwa mujibu wa Tmz, gereza hilo la Metropolitan lililopo Brooklyn limekuwa makazi ya muda kwa wafungwa mashuhuri katika miaka ya hivi karibuni, akiwemo R. Kelly, Fetty Wap, Michael Cohen, Allison Mack na Ghislaine Maxwell na sasa Diddy ambaye ataanza maisha mapya humo.

Aidha kutokana na sheria ya Marekani, msanii huyo endapo atakutwa na hatia huenda akafungwa kifungo cha maisha kutokana na mashitaka yanayomkabili likiwemo la usafirishaji wa binadamu kwa dhumuni la biashara ya ngono, njama za uhalifu pamoja na dawa za kulevya.

Kwa upande wa Marc Agnifilo ambaye ni mwanasheria wa Diddy, amedai siku ya jana mkali huyo alienda New York kwa ajili ya kujisalimisha. Pamoja na hayo alifunguka kuwa mteja wake hana hatia na mashitaka yote yaliyofunguliwa dhidi yake huku akiahidi kumpigania.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags