Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka Hong Kong, Jackie Chan amekanusha tetesi za kustaafu kuigiza, ambapo ameweka wazi kuwa ataendelea kufanya kazi hiyo kwa muda usiojulikana.
Wakati alipokuwa kwenye mahojinao mapema mwezi huu na ‘Haute Living’, amekanusha uvumi huo huku, akaeleza kuwa ataendelea kuigiza hata katika filamu zinazohusisha hatari (stunts) yeye mwenyewe.
“Kwa kweli, nitaendelea kuigiza hata kufanya filamu zile za hatari (stunts) wenyewe na haitakuja kutokea kwamwe mimi kustaafu,”amesema Chan
Akielezea kuhusu kufanya filamu za hatari Chan, ambaye ameigiza kwa zaidi ya miaka 60, alieleza kuwa uzoefu wake umemwezesha kufanya stunts bila maandalizi maalum, kwani kila kitu kiko kwenye kumbukumbu ya misuli yake.
Aliongeza kuwa, licha ya maendeleo ya teknolojia kama CGI, bado anaamini kuwa hatari halisi na uhalisia wa stunts vinatoa mvuto wa kipekee katika filamu.
Chan, ambaye alianza kazi ya uigizaji akiwa na umri wa miaka 8 kwasasa anatarajia kuonekana katika filamu ya Karate Kid: Legends kama Bw. Han, filamu inayotarajiwa kutoka 30 Mei 2025.
Akiwa na miaka 71 sasa Chan ametambulika kupitia filamu zake mbalimbali ikiwemo Rush Hour (1998), Drunken Master (1978), Police Story (1985), The Karate Kid (2010), Shanghai Noon (2000) na nyinginezo.

Leave a Reply