P Diddy anyimwa dhamana kesi ya uhalifu wa kingono

P Diddy anyimwa dhamana kesi ya uhalifu wa kingono

Mwanamuziki wa Marekani, Sean "Diddy" Combs, anayekabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kingono, anaendelea kuzuiwa kutoka mahabusi hadi kesi yake itakaposikilizwa tena.

Hakimu wa Mahakama ya New York, Robyn Tarnofsky ametoa uamuzi wa kushikiliwa mahabusu gwiji huyo wa muziki baada ya kesi yake kusomwa jana Jumanne, Septemba 17 na kukataa pendekezo la dhamana lililotolewa na mawakili wa Combs.

Mwanamuzi huyo maarufu kwa jina la P Diddy alishtakiwa kwa ulanghai wa wa kingono na usafirishaji wa makahaba ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono.

Mbali na hilo, waendesha mashtaka wamedai kuwa, P Diddy alikutwa na dawa za kulevya katika chumba cha hoteli alimokamatwa Jumatatu, Septemba 16, 2024.

Akiwa mahakamani jana, P Diddy alivalia shati jeusi la mikono mirefu na suruali ya rangi ya kijivu na kukana mashtaka yanayomkabili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags