Tiwa Savage aomba kutafsiriwa ngoma ya G-Nako Na Diamond

Tiwa Savage aomba kutafsiriwa ngoma ya G-Nako Na Diamond

Mwanamuziki kutoka Nigeria Tiwa Savage ameomba kutafsiriwa wimbo wa ‘Komando’ wa mwanamuziki G Nako na Diamondplatnumz.

Hiyo ni baada kusikia jina lake likitajwa katika wimbo huo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Tiwa alieleza kuwa nyimbo nyingi zinaimba jina lake hivyo anadhani yeye ni mtu maalumu na maarufu sana.

“Nyimbo nyingi zinatumia jina langu, naanza kuhisi kama mimi ni maalum, lakini subiri, nani anaweza kutafsiri kwa sababu natumai hawanitusi katika nyimbo zao” ameandika Tiwa Savage.

Hata hivyo kwa upande wa G Nako kupitia ukurasa wake wa Instagram alimjibu msanii huyo kwa kuwaomba mashabiki wake waweze kumtafsiria wimbo huo.

Utakumbuka kuwa wimbo wa ‘Komando’ uliachiwa rasmi Novemba 2023 G Nako alimshirikisha Diamond Platnumz, mpaka kufikia sasa video ya wimbo huo ina zaidi ya watazamaji milioni 8 katika mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags