Video Ya Diddy Akimshambulia Cassie Ilieditiwa

Video Ya Diddy Akimshambulia Cassie Ilieditiwa

Mwanasheria wa Cassie Ventura, Douglas Wigdor amefunguka kuwa hapokei visingizio vyovyote kutoka kwa Diddy, baada ya kudaiwa kwamba video ikimuonesha akimshambulia mteja wake kuwa ilieditiwa kabla ya kusambazwa mitandaoni.

Douglas ameiambia TMZ kuwa anauhakika kuwa video iliyowasilishwa itakubalika kama ushahidi mahakamani na kuwa hatosikiliza visingizio vyovyote kutoka kwa Combs.

“Sio jambo la kushangaza kwamba Diddy angeweza kutoa hoja isiyo na uaminifu ili kuzuia video inayotisha kuonyeshwa mahakamani katika kesi inayokuja. Nina uhakika kwamba video inawakilisha kwa haki na kwa usahihi kilichotokea, itakubalika kama ushahidi na kwamba Diddy atawajibishwa kwa uchafu wake,” amesema Douglas wakili wa Cassie

Nakala halisi ya video ya shambulio la Cassie na Diddy katika korido ya hoteli, ambayo ilirekodiwa mwaka 2016, inadaiwa kueditiwa na CNN ambao waliinunua miaka michache iliyopita.

Utakumbuka mapema mwezi Mei, 2024 CNN waliipandisha video hiyo kwa mara ya kwanza kupitia runinga na mitandao ya kijamii huku wakiweka wazi kuwa Diddy alitoa zaidi ya dola milioni 100 kwa hoteli hiyo ili isiweze kusambazwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags