Shah Rukh Khan Awajibu Wanaomkosoa Kisa Met Gala

Shah Rukh Khan Awajibu Wanaomkosoa Kisa Met Gala

Baada ya kupokea ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki na wadau mbalimbali katika mitandao ya kijamii kuhusiana na vazi alilolivaa kwenye ‘Met Gala 2025’, mwigizaji Shah Rukh Khan amefunguka kuwa hajali kuhusu ukosoaji huo hivyo atavaa nguo nyeusi mpaka pale watu watakapogundua uzuri wa rangi hiyo.

“Kwa sababu mimi huvaa nyeusi tu, binti yangu aliniambia kile watu wanakisema kwenye Instagram yake, hivyo Nitavaa nyeusi hadi watakapogundua rangi iliyo na giza zaidi ni nzuri sana,”ameandika Khan

Utakumbuka kuwa Khan alipata ukosoaji mkubwa baada ya kuvalia nguo nyeusi katika maonesho ya fashion na mitindo ‘Met Gala 2025’ huku wengi wao wakimnanga kuwa hajapendeza pamoja na kutoa maneno makali mbunifu wa vazi hilo.

Shah Rukh Khan ameweka historia kuwa mwigizaji wa kwanza wa kiume kutoka India kuhudhuria Met Gala. Khan alijitokeza akiwa na vazi maalumu lililobuniwa na mbunifu maarufu wa India, Sabyasachi Mukherjee, huku akitupia vito vya kifahari ikiwemo mkufu wenye herufi 'K' iliyopambwa kwa almasi, ishara ya jina lake la utani "King Khan".

Alivaa mkufu mwingine wenye herufi 'SRK', Akiwa ameshika fimbo ya dhahabu, pamoja na saa, pete za almasi.

Katika mahojiano na Time, Shah Rukh Khan alieleza furaha yake ya kushiriki katika Met Gala na kupongeza dhamira yake ya mwaka huu ambayo imelenga kusherehekea mitindo ya mavazi ya watu weusi na mchango wao katika sanaa na utamaduni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags