Kesi Inayomkabili Chris Brown Yafutwa

Kesi Inayomkabili Chris Brown Yafutwa

Kesi ya madai inayomkabili mwanamuziki kutoka Marekani, Chris Brown ya kumpiga na chupa mtayarishaji wa muziki Abe Diaw tukio lililotokea jijini London kwenye moja ya klabu ya usiku Februari 2023 yafutwa.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa Mahakamani ambazo zimepatikana na tovuti ya Billboard, Diaw siku chahce zilizopita aliomba kesi hiyo ifutwe kabisa kwa masharti ya kutofunguliwa tena ‘Dismissed With Prejudice’.

Aidha inaelezwa kuwa ombi la kufutwa kwa kesi kunaelezwa kuwa ni makubaliano kwa baina ya pande zote mbili huku kukiwa hakuna taarifa kwa wawili hao kuhusiana na tamko rasmi.

Utakumbuka Diaw alidai kuwa Brown alimshambulia mara kadhaa na chupa ya pombe aina ya ‘Don Julio 1942’ akiwa katika kilabu ya usiku ya Tape, kisha akaendelea kumkanyaga, jambo ambalo linadaiwa kumuuacha mtayarishaji huyo wa muziki majeraha na kupoteza fahamu.

Hata hivyo, Brown bado anakabiliwa na mashtaka ya jinai kuhusiana na tukio hilo. Alikamatwa katika hoteli moja mjini Manchester Mei 15 alipowasili jijini hapo kwa ajili ya mazoezi ya tamasha lake ambapo alikamatwa kwa makossa ya kusababisha madhara makubwa ya mwilini kwa makusudi, pamoja na mashtaka ya ziada ya kushambulia na kumiliki silaha.

Brown alinyimwa dhamana awali, jambo ambalo liliweka hatarini ziara yake ya ‘Breezy Bowl XX’, hadi pale mwimbaji huyo wa R&B alipopata dhamana kwa kutoa kiasi cha dola milioni 6.75, Mei 21.

Nyota wa R&B alifika katika mahakama ya London Juni 20 na kujitetea kuwa hana hatia dhidi ya shtaka la shambulio kali. Anatarajiwa kurejea mahakamani tena Julai 11, huku tarehe ya kuanza kwa kesi kamili ikiwa imepangwa kuwa Oktoba 26, 2026.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags