Lebo ya muziki maarufu duniani kutokea Afrika, Mavin Record leo Mei 8, 2025 imetimiza miaka 13 tangu ilipoanzishwa tarehe kama ya leo mwaka 2012 na mtayarishaji wa muziki lakini pia muimbaji tokea nchini Nigeria, Don Jazzy.
Mavin ambayo inatajwa kama lebo namba moja Afrika kwasasa ndio maskani ya wasanii wakubwa kama Rema, Ayra Starr, Crayon, Johnny Drille, Ladipoe, Magixx, Boy Spyce, Bayanni, na Lifesize Teddy ambao wote hao wapo chini ya lebo hiyo. lakini pia ina watayarishaji kama Don Jazzy, Altims, London, Baby Fresh, na Andre Vibez.
Ndani ya miaka 13 ya lebo hiyo imejizolea umaarufu mkubwa na kujipatia mafanikio ya kutosha kutoka kwa wasanii wake na lebo kiujumla miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na;
Mwaka 2020 jarida kubwa la muziki duniani Billboard Magazine liliitaja lebo hiyo kama moja ya milango ya kutokea kwa wasanii na muziki wa Nigeria ikitolea mfano kwa wasanii kama Iyanya, Tiwa Savage, Reekado Banks, Rema, Ayra Starr na wengine wengi ambao wamejinyakulia mafanikio kupitia mgongo wa usimamizi kutoka kwenye lebo hiyo.
Kuutambulisha muziki wa Afrobeat duniani, Lebo hiyo imefanikiwa kuutambulisha muziki wa Afrobeat duniani kupitia wasanii na watayarishaji wake ambao wameweza kutengeneza ngoma kubwa za aina hiyo ya muziki mfano Calm Down ya kwake Rema ambayo ilipata mafanikio makubwa kwenye majukwaa ya muziki ulimwenguni na kuweka rekodi mbalimbali kama kuwa ngoma ya kwanza ya Kiafrika kufikisha wasikilizaji bilioni moja kwenye jukwaa la spotify, lakini pia wimbo huo ulipata remix kutoka kwa msanii wa Marekani Selena Gomez na kuipeperusha bendera ya Afrobeat ulimwenguni.
Pia, lebo hiyo imefanikiwa kupokea tuzo kubwa kama Lebo Bora ya Mwaka kupitia tuzo za City People Entertainment Awards mwaka 2014, pia ilifanikiwa kuchukua tuzo ya Outstanding Achievement in Creative Direction in Music kwenye tuzo za TurnTable Music Awards.
Lakini pia wasanii kutoka kwenye lebo hiyo wamewahi kuwania tuzo kubwa za muziki dunia kama Grammy mfano mwaka 2025 Rema alikuw akiwania tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka kupitia albamu yake ya Heis iliyotoka 2024, Ayra Starr amewahi kuwania tuzo za Grammy 2024 kupitia kipengele cha Best African Music Performance kupitia wimbo wake wa Rush.
Kushirikiana na Lebo/kampuni kubwa za muziki duniani, Februari 26, 2024 kampuni kubwa ya muziki dunia UMG's ilitangaza kununua hisa kubwa kwenye lebo ya Mavin Record nakuchukua majukumu ya kuswatangaza wasanii wa lebo hiyo nje ya Afrika.
Kampuni hizo tayari wanafanya kazi pamoja. Mavin inasambazwa kimataifa nje ya Afrika na UMG's Virgin Music Group, huku wasanii wake kadhaa wanafanya kazi na lebo zake za Marekani, Starr na Republic, kwa mfano, na Lifesize Teddy na Interscope.

Leave a Reply