R. Kelly Adai Kuandika Album 25 Akiwa Gerezani

R. Kelly Adai Kuandika Album 25 Akiwa Gerezani

Baada ya ukimya wa miaka kadhaa akiwa gerezani mwanamuziki kutoka Marekani, R. Kelly ni kama amefufuliwa upya ambapo kwa mara ya kwanza amefunguka kudai kuwa muziki ndio ugonjwa wake huku akiweka wazi kuwa ameandika album 25 tangu afungwe.

Wakati alipokuwa kwenye mahojiano na ‘Inmate Tea with A&P’ msanii huyo aliwaburudisha mashabiki kwa kuimba sehemu ya wimbo wake wa 1998, "When a Woman's Fed Up", kisha baadaye akatumbuiza kipande cha wimbo wake wa 2003, "Step in the Name of Love."

Kelly alithibitisha kuwa hukumu yake haijapunguza mapenzi yake kwa muziki, “Kuimba ni ugonjwa mzuri usioweza kutibika, Naimba kila wakati, mpaka sasa nimeshaandika album 25 tangu niingie gerezani,”amesema Kelly

Ingawa anaonekana kuwa na shughuli nyingi gerezani ameeleza kuwa anaendelea kufanya kazi zake kutoka nje ili aweze kurejea kikamilifu kwenye Sanaa yake huku akifunguka kuwa ataongeza uvumilivu ili kufanikisha hilo, “Uvumilivu kama mbinu ya kufanikiwa”.

Aidha kupitia mahojiano hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu Kelly alisikika akifanya remix ya wimbo wa Chris Brown, uitwao ‘Residuals’ ulioachiwa 2024. Jambo hilo lilizua majadiliano katika mitandano ya kijamii huku wengi wakimkosoa Kelly kutaka kurudi mjini kwa nguvu.

“Mnamrudisha polepole Kelly kwenye muziki”, “Kwa nini R. Kelly anafanya remix ya Residuals tafadhali maliza kifungo chako kimya kimya,” “R. Kelly, Robert Kelly. Haijalishi unavyomtaja au kumweka katika muktadha gani, yeye ni mnyanyasaji wa kingono." Zimeeleza baadhi ya komenti

Utakumbuka R. Kelly anatumikia kifungo cha miaka 30 gerezani kwa makosa ya shirikisho ya usafirishajhi wa binadamu kwa ajili ya ngono na uhalifu, pamoja na miaka 20 kwa makosa ya uhalifu wa kingono huko Chicago. Hata hivyo, waendesha mashtaka wamempunguzia adhabu na kuwa atatekeleza vifungo hivyo kwa pamoja ambapo atatumikia miaka 30 jela.

Mkali huyo ambaye alikamata Julai 11, 2019, Chicago huku akianza kutumikia kifungo Agosti 2019 amewahi kutamba na ngoma kama "I Believe I Can Fly" (1996), "Ignition (Remix)" (2003), "Bump N' Grind" (1994), "Step in the Name of Love" (2003), "When a Woman's Fed Up" (1998) nk.

Hata hivyo kwa upande wa mwanasheria wa Kelly, Jennifer Bonjean, aliiambia TMZ "Nilimtembelea jana na alikuwa na hali nzuri. Si mtu aliyevunjika moyo na hakuna anayeweza kumkataa. Mchakato wetu wa rufaa haujakamilika. Tutendelea kupigania haki na uhuru wake."






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags