Mke aomba talaka kisa mumewe haogi

Mke aomba talaka kisa mumewe haogi

Mwanamke mmoja kutoka Agra, India ambaye hajawekwa wazi jina lake ameripotiwa kuomba talaka kwa mumewe ikiwa ni siku 40 tangu wawili hao kufunga ndoa, huku kisa kikiwa ni kutopenda kuoga.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘India Today’ imeeleza kuwa mwanaume huyo aliyetambulika kwa jina moja ‘Rajesh’ ameoga mara sita tu ndani ya siku 40 hali inayosababisha harufu mbaya ya mwili ambayo mkewe hakuweza kustahamili.

Kutokana na tukio hilo mwanamke huyo alipeleka malalamiko katika kituo cha ushauri nasaha cha familia kilichopo kwenye kitongoji hicho, kufuatia na mazungumzo mwanaume huyo alikubali kubadilisha tabia yake huku akiahidi kuoga kila siku.

Licha ya kutoa ahadi hiyo mwanamke huyo aligoma kabisa kurudi kwenye ndoa na kusisitiza apewe talaka yake. Hata hivyo wanandoa hao wametakiwa kurudi tena katika kituo cha ushauri nasaha Septemba 22 kwa ajili ya mazungumzo ya upatanisho zaidi.

Hii siyo mara ya kwanza kwa kitongoji cha Agra kuwepo na talaka za kustaajabu, mapema mwaka huu mwanamke mmoja aliomba talaka kwa mumewe baada ya kutonunuliwa kitoweo cha pakti kiitwacho ‘Kurkure snack’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags