Hellow! Hellow! Natumai mko pouwa eeeh watu wangu wa nguvu, naona bado siku kadhaa tuu tufike kwenye kwenye ile siku ambayo wenye wapenzi ndo wanaitamani lakini kwa sie masingle tuona kama ni siku tuu.
Oky! Tuachanae na hayo haya wanangu wa vyuoni msinichoke niko hapa kwa ajili ya kuwafanya mtumie elimu mnayo ipata chuoni kufanya kitu kitakacho kusaidia katika maisha yako.
Kama tulivyoongea week iliopita kuhusiana na kuwa mwanafunzi wa chuo kuna maana gani kwako, sijataka kuwatupa mbali sasa leo tumekuja na mada hii ili kuweza kuelewa Zaidi kuhusiana na “sababu kuu kwanini chuo ni muhimu kwako n aka maisha yako” ungana nasi mwanzo mpaka mwisho kujifunza Zaidi.
Nalikumbuka nilipopata barua yangu ya kujiunga na Chuo furaha, shauku ya kuanza kurejea tena shuleni, furaha ya kuwa mwanafunzi ilizidi ukizingatia nimesota home kwa kipindi kirefu kidogo ndipo nikapata sababu kwa nini chuo kilikuwa muhimu.
Hizi ndizo baadhi ya Sababu kwa nini Chuo ni muhimu
- Kwanza Uhuru
Hakuna furaha ambayo watu wengi huipenda katika maisha kama kuwa nje ya nyumba yaaani anytime uko huru unajifanyia maamuzi mwenyewe asikwambie mtu hii furaha ni Zaidi ya ile ya kunywa mirinda nyeusi ya baridiiii.
Kuna furaha hii inayotokana na kuwa nje ya nyumba kutokana na usumbufu na majukumu ya wazazi wako. Nje ya nyumbani, wewe ni ndo unajiongoza unaweza kwenda popote unapopataka unaweza hata kusafiri nje ya nchi bila idhini ya wazazi wako na bila ya wao kujua.
Kwangu mimi hili ndilo jambo zuri la kushangaza zaidi kuhusu maisha ya chuo kikuu kwa sababu unapokuwa huru, unaweza kufanya chochote unachotaka kufanya. Jambo lingine kuhusu uhuru ni uwezo wa kufuata ndoto zako na kufanya kile unachopenda kufanya.
- Pili kupata Marafiki wapya
Hapa katika kuongeza na kukutana na marafiki wapya Kwa kweli mtakutana na aina tofauti tofauti ya marafiki wazuri na wabaya. Wazuri watakuwa wachache sana ila jitahidi sana kuwa karibu nao maana watakuongezea thamani.
Wale wabaya mimi huwaambia watu karibu nami kila wakati marafiki wabaya hawako mbali ni watu walio karibu nawe Kwa hivyo, unachotakiwa kufanya ni kuwachambua watu wanaokuzunguka na kuwaondoa wale ambao hawaongezi thamani ya maisha yako.
Jambo moja kuhusu marafiki ni kwamba utaelewa kuwa hakuna kitu hudumu milele, kwa hivyo tumia marafiki wako zaidi ili uweze kukumbukwa kwa uzuri kila wakati.
- Tatu kupata Habari kuhusu Scholarship
Mazingira ya chuo yanafaa kwa kupata habari ya kutimiza ndoto zako za kwenda kusomea nje ya nchi ( scholarship) kwa ajili ya kuongeza ufanisi Zaidi wa kile unacho somea, so na hapa ndo utaelewa kumbe chuo ni muhimu kwasababu kitachagua uishi vipi hapo baadae.
- Nne Utapata Washauri wazuri
Umuhimu mwingine bwana ni utapata kukutana na maprofesa ambao sio wachoyo katika kutoa elimu ya maisha waliyo yapitia wanaweza kukushauri katika raundi zote za maisha, kwa mfano katika Uongozi, Tabia na ubora, hivyo basi cha kufanya ni kuwa karibu na lecture ili uweze kupata ukitakacho, waswahili wanasema kaa karibu na waridi ili uweze kunukia so washikirie.
- Tano Utapata hamasa ya Kuanzisha Biashara
Chuo ni mahali pazuri pa kuanzisha chochote, yaani kuanzisha biashara yoyote ile, cha kwanza ni kutokuangalia watu watakuonaje utakapo fanya hiyo biashara, cha kufanya ni kuzunguka mazingira ya chuo na kutazama watu wanauhitaji wa kitu gani haswa ndicho ukifanyie biashara.
Mfano mimi katika chuo nilichosoma vyakula vinavyopikwa canteen vilikuwa ni vibovu so nikaamua kuwa ntakuwa napika chakula nawauzia wanafunzi wenzangu, hata kama ni karanga, ubuyu wewe uza tuu hii yote ni kwaajili ya kusave pesa zako ili ziweze kukusaidia kwa mambo yako madogo madogo.
Cha kuzingatia katika kuanzisha hiyo biashara ni kukwepa biashara yako isiingiliane kabisa na taaluma yako ya masomo ukashuka kwa sababu ya pesa. Kama kweli kwenu umetumwa pesa ndipo utajua kuwa eneo hili nikifanya biashara itatoka.
- Mwisho, chuo ni mwanzo wa maisha yako
Kwanini nasema chuo ni mwanzo wa maisha yako kwasababu ukiharibu basi umeharibu mtazamo wako mazima, kuna baadhi ya watu wanadanganyana sana kuwa “kusoma sio kufaulu’ wengine utawaskia “ wakusoma tutakuwa sie” my friend hizi kauli zitakupotosha sana.
Kuna baadhi ya wanafunzi kauli hizi huzichukulia kama mzaha tuu lakini kuna baadhi ya watu huchukulia kauli hizi ni ukweli basi hawa ndo ukija kutazama matokeo yao hamna kitu kabisa, chuo bwana hutakiwi kumuamini mwanafunzi mwenzio eti akwambie mimi sijasoma na ni siku ya testi na wewe ukasema usisome ndugu yangu utajikuta wewe wamwisho kila siku.
Chuo ni maisa yako kwasababu ni sehemu ya kukutana na watu tofauti tofauti watakao kusaidia ukapata kazi pale tuu umalizapo chuo, so usichukulie chuo ni mzaha hayo ndo maisha yako, huo ndo ugali wa wanao baadae, ili usije kujuta baadae zinduka sasa.
Haya haya amkeni amkeni ni kama nimewachosha hivi lakini sio sana bwana, hayo ni mambo machache tuu ya kukuzindua wewe ndugu yangu na kujua chuo ni muhimu katika maisha yako, wewe kijana mwenzangu usichukulie mzaha na kuona kuwa mimi nakudanganya lakini hapo baadae utakuja kunikumbuka japo sio baba wa taifa.
Leave a Reply