Mwaka 2024 mtamu kwa Ibraah

Mwaka 2024 mtamu kwa Ibraah

Na Masoud Koffie

Mwanamuziki Ibraah ambaye amesainiwa chini ya lebo ya Konde Gang Music Word Wide, kwa sasa tunaweza kumuita nyota wa mchezo kwenye muziki wa Bongo Fleva, hii ni kutokana na namna ambavyo amefanya kwenye ngoma tofauti zikiwemo za kwake na hata zile alizoshirikishwa 

Ibraah kwa mwaka 2024 mchango wake umekuwa mkubwa kwenye Muziki wa Bongo Fleva kutokana na kufanya ngoma mfululizo tangu mwezi Februari alipoachia Wimbo wa Dharau aliomshirikisha Harmonize ukiwa umetazamwa zaidi ya mara milioni 13 kwenye Mtandao wa Youtube huku ukiwa haujawahi kutoka kwenye trendi ya nyimbo 30 tangu kuachiwa kwake. 

Kwa mwaka 2024, Ibraah ameshirikiana na wasanii mbalimbali na kila wimbo alioshirikishwa umefanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii, mfano wa nyimbo hizo ni "Amen" aliyoshirikishwa na Msamiart, "Niposingle" aliyoshirikishwa na Dayoo, "Hakunaga" aliyoshirikishwa na Vannilah, "Tangazo" ya kwake Kontawa, "Kariako" ya kwao Maua Sama, G Nako ft Jaiva na hata inayokimbiza kwa sasa "Wivu" ya Dj Mushizo. 

Msanii huyu wa kwanza kusainiwa Konde Gang, ameonekana kuendelea kuwateka mashabiki wengi hivi karibuni kutokana na verse yake inayosikika mwanzoni mwa wimbo wa "Wivu" ambao ndani yake yumo Dj Mushizo, Jay Combat na Baddest. 

Sababu zinazomfanya Ibraah kuonekana nyota wa mchezo kipindi hiki ni kutokana na anavyohitajika zaidi kwenye kukamilisha baadhi ya ngoma za wasanii wenzake, tunaweza kusema mwaka 2024 umemuendea vizuri kwenye muziki lakini kazi nyingi alizofanya na zilizomuweka juu ameshirikishwa hiyo yote ni kuonekana na mchango kwenye game.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags