Zuchu afanya kolabo na Yemi Alade

Zuchu afanya kolabo na Yemi Alade

Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Zuchu huenda akawa amefanya kolabo na mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria Yemi Alade, hii ni baada ya kuweka wazi kuwa kunamteule kwenye tuzo za Grammy katika album yake.

Zuchu ameyasema hayo kupitia Instastory yake kwa kuchapisha picha ya Yemi huku akimpongeza kwa kuteuliwa kuwania tuzo hizo na kubariki album yake.

“Hongera kwa malkia kwa uteuzi wa Grammy, asante kwa kubariki albamu yangu kwa talanta yako, tunamteule wa Grammy kwenye albamu yetu”, ameandika Yemi

Utakumbuka kuwa Zuchu alitangaza ujio wa album yake mwezi June huku mpaka kufikia sasa ameeleza kuwa album hiyo ipo tayari kwa asilimia mia na huenda akaiachia muda wowote kutoka sasa.

Endapo albumu hiyo itafanikiwa kuachiwa itakuwa ya kwanza kwa Zuchu. Mwaka 2020 mwanamuziki huyo alifanikiwa kutoa EP yenye nyimbo saba ambayo ndiyo iliyomleta mjini.

EP hiyo ya Zuchu iliyopewa jina la ‘I Am Zuchu’ ikiwa na nyimbo kama ‘Hakuna Kulala’, ‘Nisamehe’, ‘Wana’, ‘Ashua’, ‘Kwaru’, Raha’ na ‘Mauzauza aliyomshirikisha Mama yake Khadija Kopa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags