Vitu 10 Mwanachuo anapaswa kuvifanya mapema

Vitu 10 Mwanachuo anapaswa kuvifanya mapema

Kipindi uko chuo ni kipindi ambacho una mambo mengi ya kufanya kwaajili ya masomo lakini pia muda mwingine una muda mwingi ambao unaweza ukauwekeza kwenye kujiendeleza wewe mwenyewe mbali tu na kuwa unaangalia series kila siku.

Leo naenda kushare mambo 10 ambayo unapaswa kuanza kuyafanya mapema toka ukiwa chuo;

  1. Kuweka akiba

Ukiwa chuo ndio muda mzuri wa kujifunza kuweka akiba, muda mzuri wa kujifunza kuwa na matumizi mazuri ya hela.

Hasa kama unapata boom au una biashara unayoifanya inayokuingizia pesa, usitumie hela vibaya chuoni, ukiweka akiba inaweza kukusaidia hata ukimaliza chuo ukawa na nauli za kwendea kwenye interviews.

Haya hapa ni matumizi mabaya ya pesa niliyoyafanya nikiwa chuoni, nimeshare ili wewe usikosee nilipokosea.

  1. Kujiandaa na maisha ya mtaani

Njia rahisi na ambayo nimeshaitaja ndio kama hiyo, kuweka akiba ili ukimaliza chuo na ukawa umeingia mtaani hauna hela uwe hata na kiasi kinachokusukuma.

Njia nyingine ni kufikiria kuhusu maisha yako baada ya chuo, wengi tunawaza utapata kazi, ila kaa chini fikiria mambo yote, vipi kama usipopata? Vipi kama ukichukua muda kupata kazi? Utaishi wapi? Umetengeneza CV nk.

  1. Kutengeneza mahusiano mazuri na watu

Hasa wanafunzi wenzio. Kuna maisha baada ya chuo. Kuna wale watakaoshare fursa na wewe, watakaokusupport utakayoyafanya baada ya chuo na wale watakao kuwa nawe kwenye maisha baada ya chuo.

Tengeneza mahusiano mazuri na watu, sio wote maana usije ukawa unajipendekeza tu ila hakikisha una watu wanaokuthamini na unaowathamini, na pia usipopata watu wa hivyo chuoni hakuna shida pia.

  1. Kusoma vitabu

Kuna maarifa tofauti na yale ya darasani unayoweza kuyapata kwenye vitabu. Soma vitabu vya topic mbalimbali tofauti na vya chuo ili ujifunze kuhusu maisha.

  1. Kujitambua (kujitafuta)

Muda huu ambao uko peke yako, unaingia kwenye utu uzima, ni vizuri kuutumia kujitafuta, kujifunza kuhusu wewe, kujitambua, misimamo yako, nini unapenda, njia gani unapenda kuishi maisha yako usiwe tu mfuataji wa trends.

(Usiache Kusubscribe YouTube channel ambayo ninashare dondoo za Maisha ya Chuo kila Alhamisi na pia Kufollow Instagram page ya Maisha ya Chuo ambapo kila siku nashare dondoo kwaajili ya wanachuo)

  1. Kufikiria project watakazozifanya

Ni vizuri kuanza kufikiria kuhusu project unayotamani kuifanya ukiwa chuoni mapema, kuliko kukurupuka kuchagua wakati muda umefika wa kupresent.

Soma hapa kujua vitu unavyotakiwa kuzingatia unapochagua project ya kufanya chuoni

  1. Kujali afya zao

Ukiwa unaumwa hauwezi kusoma. Jali afya yako, kunywa maji, fanya mazoezi, usikae tu kitandani na kula chipsi. Kula vyakula vyenye virutubisho.

  1. Kujitolea sehemu unazoona wanafanya mambo unayoyapenda

Au kufuatilia kazi zao pia. Unaweza kujitolea weekend, kwa masaa nk. Ila jioneshe kwenye hizo sehemu mapema ili hata ukimaliza unaweza kuwa na nafasi na hata usipokuwa nayo umepata experience.

  1. Kujifunza vitu vipya tofauti na kozi zao hasa vitu wanavyovipenda

Kuna watu wamemaliza chuo na kuacha kufanyia kazi walichosomea, jifunze vitu vingine. Kama ni graphic designing, kama ni kupiga picha, kuchora nk. Make sure unaikuza hobby yako pia.

  1. Kufikiria kama mahusiano yao ya kimapenzi ni ya kweli au yanawapotezea tu muda

Muda mwingine tunaingia kwenye mahusiano kwasababu zisizo nzuri. Hasa chuo, unaweza kuingia kwa peer pressure, trend, au sababu yoyote ile.

Ukiwa chuo ni vizuri kujichunguza kama kweli hayo mahusiano yanasababu na yanaelekea sehemu au unajiumiza moyo na kupoteza muda.

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post