Kwa mujibu wa Sensa Uingereza, idadi ya Wakristo yashuka England na Wales

Kwa mujibu wa Sensa Uingereza, idadi ya Wakristo yashuka England na Wales

Kwa mara ya kwanza nchini Uingereza takwimu za sensa ya watu na makazi zimeonesha, chini ya nusu ya idadi ya watu England na Wales ni wakristo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa Jumanne, sensa ya kipindi cha miaka 10 iliyofanywa mwaka jana 2021 inaonesha ongezeko kubwa la watu wenye kufuata dini ya kiislamu,ikifuatiwa na watu wasiokuwa na dini.

Takwimu hizo zimetolewa na ofisi ya taifa ya Tawimu ONS. Moja ya masuali yaliyoulizwa katika zoezi hilo la kuhesabu watu ni kuhusu dini na ambalo kimsingi liliorodheshwa katika utafiti huo tangu mwaka 2001 likiwa ni suali la hiari. Hata hivyo asilimia 94.0 ya watu walijibu suali hilo kwa mujibu wa ONS.

Askofu wa York Stephen Cottrell amesema matokeo hayo hayashangazi sana kuona idadi ya wakristo imekuwa ikiteremka kadri muda unavyokwenda. Ingawa ameongeza kusema kutokana na mgogoro wa ughali wa maisha na vita barani Ulaya, watu bado wanahitaji kuendelea kushikilia imani ya kiroho.

Wakristo watajwa kuwa watu kiasi milioni 27.5 England na Wales idadi ambayo inaonesha imeshuka kwa aasilimia 13.1 kutoka mwaka 2011. Idadi ya Waislamu imeongezeka kutoka asilimia 4.9 hadi asilimia 6.5.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post