Fanya haya kumove on unapomwagana na mpenzi wako wa chuoni

Fanya haya kumove on unapomwagana na mpenzi wako wa chuoni

Uwiiiiiiiih! Unajua kuachwa wewe sio pouwa kabisa, I hope mko good watu wangu wa nguvu, leo nimewaletea mada najua wengi mtakuwa nayo attention coz mshapigwa na vitu vizito kadhaa.

Kuachana na mpenzi wako ni jambo gumu kulipitia katika sehemu yoyote, ila nahisi ukiwa chuo ugumu unaongezeka kwaajili ya ukaribu na kwa vile mnaonana mara kwa mara labda darasa moja au kwa vile chuo  kimoja basi lazima mtaonana na hio kiaina itakuumiza na kukushelewesha kuweza kusahau.

Na share na nyie experience ambayo rafiki yangu alikuwa anaifanya baada tu yakuachana na mpenzi wake, kwakuwa tuko karibu sana alikuwa ananieleza kila kitu ndipo nikapata kujua.

Na haya ndo mambo ya kuyafanya ili uweze kumove on kwa haraka zaidi.

  • Kwanza usiingie kwenye mahusiano kutafuta uponyaji

Wengi huwa wanahisi kumove on maana yake kuwa na mtu mwingine, kumove on ni kutokuumia tena na kusahau mambo yote mliowahi kuyafanya pamoja na ex wako.

Kosa ambalo wengi wanalifanya/tunalifanya ni kukimbilia mahusiano mengine chap chap labda ya kutafuta uponyaji au ili kuonesha  tumemove on’ na hatuumii tena kuhusu yeye.

Unaweza fanya uchaguzi mbaya wa huyo mtu mpya kwasababu ya haraka ya kupona maumivu uliosababishiwa hapo awali, my wangu usijaribu kabisa kufanya mambo kama haya maana huyo unayemuona ni sahihi kwako akaja kukutonesha kidonda zaidi ya yule wa mwanzao. Waswahili tunasema ukiachwa achika na subiri karma ya Mungu itakuandikia kitu gani usikurupuke.

  • Pili wekeza nguvu na hasira kwenye masomo

Najua watu wanapitia/tunapitia hali tofauti baada ya kuachana na wapenzi wetu, wengi hupata sonona na kuchanganyikiwa  kabisa, kuachana na mtu siyo jambo jepesi, cha muhimu ni kuachana na hizo mambo na kuzinduka kwa kujua kilichokupeleka chuoni.

Ila kama hauna sonona wala haujachanganyikiwa kwa namna yoyote ile basi tumia hiyo hasira na nguvu uchungu uliyonayo kuuweka kwenye masomo yako. Unaweza kutumia kuachana kama jambo lililokushtua na kukuamsha na kukuonesha jambo gani ni la msingi na lililokuleta chuo ambalo ni kusoma. Fanya kama ni jambo la kupita tuu katioka maisha.

  • Tatu kuwa na mtu wa kuongea naye

Unaweza ongea na washauri wa chuo, mwanafunzi mwenzio au mtu yoyote ambaye anaweza kuwa msaada kwako. Kuongea kunasaidia kutoa uchungu, kuna kusaidia kuangalia hali yako kwa jicho jingine lakini pia kutua mzigo.

Kama nilivyosema hapo awali, mimi rafiki yangu alikuwa ananieleza kila kitu na akishaeleza vile mwenyewe alikuwa anasema anajisakia vizuri kuliko kuamua kukaa nalo moyoni basi tafuta msiri wako na umueleze kila jambo.

  • Nne usiweke uzito au kufikiria watu wanakufikiriaje

Ubaya wa chuo ni kuwa watu wanapenda drama, udaku na kuongelea wengine vibaya na kwa vile labda watu walikuwa wanajua kuhusu uhusiano wenu, ni rahisi sana kuachana kwenu kukawa mada kati ya watu waliokuwa wanajua. 

Cha msingi cha kufanya ni usifikirie watu wanazungumza nini ama wanakuonaje, huwa inaumiza lakini pia inakufanya uwe mtumwa wa mawazo yao, kila saa unawaza wanakuonaje na hili ndo jambo litakalo kuchelewesha kupona lakini usijali chochote.

Hawakuwa kwenye mahusiano yenu kwahiyo hawajui ukweli wote lakini pia kama unaona hakuna umuhimu sio lazima ujieleze sana kwao. Maisha ni yako ni yako, usijali watu wanaongea nini.

  • Tano punguza kumuona au kufuatilia maisha ya ex wako

Ukimfuatilia ukajua kuhusu maisha yake haikusaidii sana zaidi ya kukurudisha chini hatua mbili kwenye ngazi ya uponyaji. Kama unaweza kupunguza kumuona pia itakuwa vizuri, yaani punguza mazoea kabisa, vijana wa mjini tunaita shobo zipungue kabisa yaani.

Likija swala la kujali moyo wako fanya lile unaloona linakusaidia hata kama ni kumunfollow na kumblock mitandaoni, kufuta namba, kubadilisha marafiki mliokuwa mnashea nk, lolote linalokusaidia wewe fanya. Umeamua kuwa na maisha yako basi na yeye muache na maisha yake.

  • Sita jiruhusu kuumia kwa ajili ya kupoteza huo uhusiano

Wengi wetu tunataka kumove on, tusihisi hisia yoyote, ila ukweli ni kuwa unapona kwa kujiruhusu kusikia zile hisia na kuziachilia. Kama unajisikia kulia, chukua muda liaa weeeeh mpaka basi, kama unajisikia kuandika hisia zako chini fanya hivyo, usizikimbie hisia, zitarudi, jiruhusu kuumia kwa muda ili upate uponyaji wa kweli.

Lakini pia katika kuumia unaweza kujifunza kuhusu wewe au kuhusu huo uhusiano ulioisha, ukifanya hivi utakuja nishukuru baadae, maana unaondoa maumivu kwenye moyo na kuupatia moyo wako space ya kufikiria jambo jingine.

  • Mwisho fanya mambo yaliyokuwa yanakuletea furaha kabla ya kuwa naye.

Mahusiano muda mwingine hufanya tujisahau, tuhisi hatuwezi kuwa na furaha bila ya kuwa na huyu mtu kwenye maisha yetu, moja ya woga au ugumu wa kuachana ni mawazo ya jinsi gani unavyoweza kuwa na furaha wakati huyu mtu hayupo tena kwenye maisha yako.

Njia mojawapo ya kulishinda hili ni kujikumbusha na kufanya mambo yaliyokuwa yanakuletea furaha wakati bado haujaingia kwenye huo uhusiano au kutafuta mambo mapya ambayo unapenda kuyafanya yanayokuletea furaha.

Haya haya watu wangu wa nguvu, nakuhakikishia ukiamua kufanya haya niliokueleza hapo juu basi mwezi hauishi ushasahau hayo mahusiano kabisa, jambo jingine la msingi kabisa ni kumuomba Mungu maana ndo kila kitu katika haya maisha.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post