Messi afungua studio aipa jina la alipozaliwa

Messi afungua studio aipa jina la alipozaliwa

Nyota wa kimataifa wa soka, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Inter Miami CF na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi ameripotiwa kufungua studio aliyoipa jina la ‘525 Rosario’.

Messi amefungua kampuni hiyo ya maudhui akishirikiana na ‘Smuggler Entertainment’ ambayo itatengeneza na kuzalisha vipindi vya televisheni, filamu za hali ya juu, michezo ya moja kwa moja, na matukio ya kijamii.

“Burudani imekuwa shauku yangu daima, iwe uwanjani au katika nyanja nyingine. Ninapata motisha kutokana na fursa ya kufuata mradi tuliounda na ‘Smuggler Entertainment’ na kuupanua zaidi ili kuunda maudhui na uzoefu kwa kiwango cha kimataifa kupitia mradi huu mpya.” Messi ameiambia tovuti ya Variety

Mbali na hayo aliweka wazi maana ya jina la chaneli hiyo ‘525 Rosario’ ambapo Rosario ni jina la mji alipozaliwa nchini Argentina huku 525 ikiwa ni namba ya nyumba ya familia ya Messi.

525 Rosario yenye makao makuu Miami na Los Angeles, itakuwa chini ya usimamizi wa familia ya Messi na Tim Pastore, mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa Smuggler Entertainment, ambaye atahudumu kama Afisa Mtendaji Mkuu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags