Filamu Ya 28 Days Later yarekodiwa kwa kutumia Iphone 15

Filamu Ya 28 Days Later yarekodiwa kwa kutumia Iphone 15

Mwendelezo wa filamu maarufu ya ‘28 Days Later’ inayotarajiwa kutoka mwaka 2025 imeripotiwa kurekodiwa kwa kutumia simu ya Iphone 15 jambo ambalo limefanya mashabiki wahoji kuwa huwenda isiwe na ubora wa kutosha .

Filamu hiyo ya Zombie inayoongozwa na Danny Boyle imechezwa na waigizaji maarufu kama Cillian Murphy, Jodie Comer, Aaron Taylor-Johnson, na Ralph Fiennes.

Hata hivyo kwa mujibu wa Wired, imeeleza kutokana na teknolojia kunauwezekano mkubwa wa siku zijazo kupunguza bajeti katika ku-shoot ambapo filamu hiyo imedaiwa kutumia bajeti ya dola milioni 75.

Aidha kwa mujibu wa Google hii siyo filamu ya kwanza kurekodiwa kwa kutumia simu, filamu ni pamoja na Sleep Has Her House ikiongozwa na Scott Barley, High Flying Bird (Steven Soderbergh), Midnight Traveler (Hassan Fazili) na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags