Kinachoendelea kwa mastaa waliokuwa karibu na Diddy

Kinachoendelea kwa mastaa waliokuwa karibu na Diddy

Ikiwa zimepita siku nne tangu mkali wa Hip Hop kutoka Marekani Sean “Diddy” Combs, kutokuwepo uraiani, baadhi ya mastaa wameibuka katika mitandao ya kijamii wakidai kuwa wanajutia ukaribu wao na mwanamuziki huyo.

Kwa mujibu wa Daily Mail imedaiwa kuwa mwananmuziki Justine Bieber ambaye alikuwa akimuangalia Diddy kama Role Model wake anajutia ukaribu alioweka na ‘rapa’ huyo wakati anaaza kufanya muziki akiwa na miaka 14 huku ikidaiwa kuwa toka Diddy akamatwe Bieber amejifungia ndani na kusitisha mawasiliano na watu wengine zaidi ya familia yake.

Mbali na huyo naye msanii wa wazamani wa lebo ya ‘Bad Boys’, ambaye kwa sasa anajihusisha na masuala ya kisiasa Shyne alifunguka kuwa Diddy ndiye aliyechangia kuharibika kwa maisha yake wakati alipokuwa na miaka 18.

Mwanasiasa huyo alikumbushia tukio lililotokea mwaka 1999 ambapo alisema kuwa wakati wa tukio la kupiga risasi klabuni mwaka huo yeye alimtete Diddy mahakamani lakini Combs alitoa ushahidi dhidi yake na kupelekea atumikie kifungo cha miaka 10 gerezani.

Mbali na hao baada ya siku chache kupita tangu Combs akamatwe aliyekuwa mpenzi wa Diddy, Cassie ameonekana kuwa na furaha huku akiripotiwa kutoka out za mara kwa mara kwa siku za hivi karibuni, ambapo picha na video zilimuonesha akitabasamu wakati wa mtoko wa usiku huko New York.

Mwanamuzi huyo alikamatwa Jumatatu, Septemba 16, 2024 na kushitakiwa kwa makosa matatu ulaghai wa kingono, usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara hiyo ya ngono.

Mbali na hilo baada ya vyombo vya sheria kupata zaidi ya chupa 1,000 za mafuta ya watoto na vilainishi katika nyumba ya mwanamuziki huyo, wataalamu wa masuala ya tendo la ndoa wametoa onyo kuwa kutumia mafuta ya watoto kwenye tendo la ndoa yana madhara kiafya.

Baadhi ya wataalamu kutoka Las Vegas wamesisitiza kuwa haifai kutumia mafuta kama vilainishi katika tendo la ndoa kunaathiri afya ya uke na uwezekano wa kuharibu uimara wa mipira ya kondomu wakati wa tendo.

Mbali na hayo waliweka wazi kuwa kutumia mafuta ya watoto kunaweza kuvuruga uwiano wa PH kwa mwanamke na kuongeza hatari ya kupata bakteria aina ya ‘Vaginosis’. Aidha walimalizia kwa kudai pia kunaweza kusababisha mimba zisizotarajiwa na maambukizi ya zinaa, kwani yanaweza kuharibu mipira ya kondomu kwa kupasuka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags