Talaka sio vita, Jennifer Na Ben waonekana pamoja

Talaka sio vita, Jennifer Na Ben waonekana pamoja

Mwanamuziki Jennifer Lopez na aliyekuwa mumewe Ben Affleck wameendelea kuonekana pamoja licha ya wawili wao kutarajia kupeana talaka.

Lopez na Ben walionekana pamoja katika usiku wa kufunga shule ambayo wanasoma watoto wao, huku kila mmoja akionekana kuwa mkarimu na jasiri mbele ya mwenzake.

Kutokana na ukaribu wao chanzo cha karibu cha wanandoa hao wa zamani kiliiambia Tmz kuwa licha ya talaka yao kuendelea kusikilizwa mahakamani lakini wawili hao bado wanaonekana kujaliana sana.

Lopez ana watoto mapacha waitwao Emme na Max (16) aliowapata na aliyekuwa mumewe Marc Anthony, naye Ben ni baba wa watoto watatu ambao ni Violet (18), Seraphina (15) na Samuel (12) aliozaa na mke wake wa zamani Jennifer Garner.

Hii siyo mara ya kwanza kwa wawili hao kuonekana wakiwa wote kwani mwishoni mwa wiki iliyopita Lopez na Ben walionekana pamoja na watoto wao katika Hoteli ya Beverly Hills huku mashihida wakidai kuwa waliwaona wawili hao wakibusiana na kushikana mikono.

Hao siyo wanandoa wa kwanza kukutana mara kwa mara licha ya kuwasilisha talaka makamani ‘rapa’ Cardi B na mzazi mwenzake Offset wamekuwa wakionekana pamoja mara kwa mara licha ya wawili hao kuwasilisha madai ya talaka mahakamani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags