Jina Abaya naimani siyo geni masikioni mwako hasa katika msimu huu wa Ramadhani. Licha ya watu wengi kusikia jina hilo wapo ambao hawafahamu ni vazi la aina gani na utamaduni wake ni upi. Fahamu zaidi
Abaya ni nini?
Abaya ni mavazi ya wanawake yanayotumika sana katika tamaduni za Kiislamu, hasa katika nchi za Mashariki ya Kati, kama vile Saudi Arabia, Emirati, na nchi nyingine za Ghuba. Abaya ni gauni refu na la kupendeza, linalofunika mwili wote kutoka kwenye mabega hadi chini. Hivyo ni mavazi yanayofunika mwili na kutunza heshima ya mtu hasa katika upande wa kujistiri.
Historia ya abaya
Abaya ina mizizi yake katika tamaduni za Kiarabu, na imekuwa sehemu ya mavazi ya kila siku kwa wanawake katika maeneo mengi ya Mashariki ya Kati kwa karne nyingi. Neno "abaya" linatokana na neno la Kiarabu linalomaanisha "nguo" au "vazi." Katika karne za zamani, abaya ilivaliwa, ikiwa ni ishara ya unyenyekevu.
Muundo wa abaya
Abaya inaweza kuwa ya rangi yoyote. Inaweza kuwa na muundo wa moja kwa moja au iliyopasuliwa katikati. Kawaida hutengenezwa kwa kitambaa kizito. Abaya pia inaweza kuwa na mapambo ya aina mbalimbali kama vile vitu vya mng'ao, michoro na vinginevyo.
Abaya na Hijab
Katika baadhi ya maeneo, abaya inavaliwa pamoja na hijab – vazi linalofunika nywele na shingo ya wanawake Waislamu ili kuhifadhi na kuficha mwili. Katika maeneo mengine, baadhi ya wanawake pia huvaa niqab au burqa, ambao hufunika uso kabisa.

Leave a Reply