Mbinu za Kudhibiti Smartphone yako

Mbinu za Kudhibiti Smartphone yako

 

Mpooo!!!? Alaaaah!Ni wiki nyingine tena ndani ya kipengele chako cha kibabe cha Smartphone karibu kwenye ukurasa huu bhana kama kawa kama dawa leo nakuletea namna utakavyoweza kudhibiti simu yako.

Aiseee yaani namaanisha hakuna mtu atakayeweza kuja kuichezea kizembe tu bila ya ruhusa yako komaa na kipengele hiki ujifunze zaidi karibuu.

Kama unavyojua mwanangu simu janja ni muhimu kinyama kwani zinabeba taarifa nyingi hususani nyeti hivyo basi jambo la kwanza la muhimu unapomiliki simu aiana yoyote unatakiwa uwe na uwelewa wa kudhibiti taarifa zako kwenye simu.

Nikwambie tu kuwa taarifa zako zinaweza kuwa namba za simu, akaunti zako za mitandao, sauti, nyaraka, picha hata video pia lakini pia taarifa inaweza kuwa chochote huwezi kujua mtu mwingine anaweza kuitumia taarifa ya aina ipi ili kukuvuruga kuwa makini twende sawaa.

Weka password

Jambo la kwanza ambalo unaweza kulifanya kwa ajili ya usalama wa simu yako ni hilo la kuweka pattern yaani namba ya siri (PIN) ambayo ufunguo wake unao wewe tu, ufahamu wa uso (face recognition) au hata alama ya kidole( touch ID) kwa wale wenye simu za beiii.

Unganisha simu yako na huduma ya kutafuta simu

Hapa sasa ili kudhibiti simu yako hakikisha unajiunga na huduma ya kutafuta simu yako, huduma hizi ni pamoja na Android device manager, Apple i-Cloud Windows find my phone, Avast Free Security na nyinginezo ambazo hutumia ramani kutafuta simu yako iliyoibiwa iwapo tu ikiwashwa na kujiunga na intaneti.

Weka cover na screen protector

Huu sasa ndiyo ujanja mwengine nakupa tumia kasha au cover kujistiri ukiwa kwenye kadamnasi zipo aina nyingi za kava ikiwemo ( privacy cover) ndiyo inayozungumziwa hapa kava kama hizi zinapunguza  mwanga unaoonekana kwa mtu wa pembeni ili asione unachofanya kwenye simu, nunua cover ya plastiki inayoganda kwenye screen ili isichubuke au unaweza kununua cover ya kioo ili kuzuia kioo kisiharibike.

Exactly nafikiri hadi hapo tutakua tumefahamiana vyakutosha bhanaa always ni jikumu letu kukupa mambo muhimu kwa ajili ya smartphone yako keep watching our pages!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post