Msiba wa Tesa wamuibua Ray C, awataja bongo fleva

Msiba wa Tesa wamuibua Ray C, awataja bongo fleva

Mwanamuziki mkongwe nchini Rehema Chalamila ‘Ray C’ amewapongeza wasanii wa filamu nchini kwa umoja wao katika matatizo huku akiwataka wasanii wa Bongo Fleva kuiga hilo.

Ray C ameeleza hayo kupitia ukurasa waka Instagram ikiwa ni siku ya tano tangu mwigizaji Grace Mapunda ‘Tesa' wa Huba kufariki dunia, huku kwenye msiba wake wasanii wengi wa maigizo wakionekana kujitokea

“Wasanii wa Bongo Movie mna umoja sana hongereni sana, mmebeba huu msiba ipasavyo na uhakika hata Grace amepumzika akitabasamu mmewapa amani ya moyo hata wanafamilia, hongereni sana Wasanii wa Bongo Fleva kuna cha kujifunza hapa”, ameandika Ray C



Hii sio mara ya kwanza kwa wasanii wa Bongo Fleva kudaiwa kutokuwa na umoja pamoja na kutoshirikiana na mastaa wenzao kwenye matatizo, utakumbuka kuwa siku mbili zilizopita mwigizaji mkongwe nchini Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ aliwataka wasanii wa Bongo Fleva wajitokeze kwenye misiba ya wasanii wenzao.

“Wasanii wa Bongo Fleva wajitokeze kwa wingi kushirikiana na wenzao, wengi hawajitokezi kuzika, wengi hawajitokezi msibani lakini ukitokea msiba wa Bongo Fleva utawaona wasanii wetu wa Bongo Movie wote.

“Moja ya kitu tulichobahatika ni kuwa wasanii wa bongo movie wanaupendo na hofu ya Mungu na ndio maana wanakimbiliana kwenye matatizo, kwa hiyo nawasihi sana wasanii wa Bongo movie kuwa wanaokukimbilia kwenye matatizo nawe mkimbilie”, amesema Steve Nyerere

Tesa alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 2, 2024 na kuzikwa Novemba 4, 2024 kwenye makaburi ya Kinondoni, kwa maradhi ya Nimonia, Kisukari na mchafuko wa damu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags