Burna Boy kama Rayvanny tu

Burna Boy kama Rayvanny tu

Msanii wa Afrobeat kutokea Nigeria, Burna Boy ameingia kwenye trend baada ya kufanya remix za nyimbo hit kutoka kwa wasanii tofauti tofauti.

Hii ni baada ya Burna Boy kuvutiwa na wimbo wa 4 Kampe, wa Joé Dwèt Filé ambapo orijino ya wimbo huo ulitoka Oktoba 31, 2024 video yake ikitazamwa zaidi ya mara milioni 63 kwenye mtandao wa YouTube.

Burna Boy ameamua kufanya remix ya wimbo huo ambao ametoa leo Machi 28, 2025 akiwa na Joé Dwèt Filé. Hii ni kufuatia wimbo huo kuwa na miondoko ya Burna Boy hususani sehemu ya kiitikio ambapo sauti za wimbo orijino zimefanana na Burna kiasi ambacho mashabiki wengi hapo awali walidhani ameimba yeye.

Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa mkali huyo wa Afrobeat kurudia nyimbo hit za wasanii kwani amewahi kufanya hivyo kwenye wimbo wa 'Tshwala Bam' wa kwao TitoM na Yuppe moja kati ya hitsong za mwaka 2024. pia, mwaka 2020 alifanyia remix hit ya 'Jerusalema' Master KG, amerudia wimbo wa Sungba ambayo iliachiwa 2022 kutoka kwa Mr. Money with Vibe, Asake

Mwaka 2022, Burna Boy alihusika katika remix ya 'Second Sermon' ya kwake Black Sherif ngoma ambayo inapatikana kwenye album ya mkali huyo tokea Ghana, 'The Villain I Never Was', mwaka 2021 Burnaboy aliibuka kwenye ngoma ya 'Yaba Buluku' ya kwake Dj Tarico, amerudia pia ngoma ya 'Do I' Phyno iliyotoka 2024 na nyingine nyingi.

Ukiachana na Burna Boy kutisha kwenye remix za nyimbo za wasanii wengine pia amefanikiwa kutengeza hitsong zake binafsi kupitia nyimbo kama Kilometer, Big Seven, City Boy, On The Low,. Tested, Approved & Trusted, Common Person na nyingine nyingi.

Utaratibu huo ambao amekuwa nao Burna wa kudandia ngoma hit na kuzifanyia remix umezoeleka kwa msanii wa Bongo Fleva, Rayvanny ambaye mpaka alipokea vijembe kutoka kwa mashabiki wa muziki na wadau mbalimbali wakisema anatembelea upepo wa nyimbo hit kutoka kwa wasanii wengine.

Rayvanny amefanya remix kwenye ngoma kama Distance ya Jay Rox, Gibela ya Chino Kidd akiwa na S2kizzy & Mfana Kah Gogo, Jennifer ya Guchi, How Low ya KashComing, Kitu Kizito ya Misso Misondo, Sukuma Ndinga ya Rosa Ree na nyingine nyingi.

Kwa upande mwingine Rayvanny amekuwa mwandishi mzuri wa nyimbo zake binafsi na amefanikiwa kupata hitsong nyingi ikiwa ni pamoja na Sensema, Nesa Nesa, Kwetu, unaibiwa, Amaboka na nyingine nyingi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags