Msanii Young Scooter afariki kwa kupigwa Risasi

Msanii Young Scooter afariki kwa kupigwa Risasi

Rapa tokea jiji la Atlanta nchini Marekani, Young Scooter anaripotiwa kufariki dunia kutokana na majeraha yaliyosababishwa na kupigwa risasi wakati wa mzozo kwenye moja ya nyumba jijini humo.

Scooter amefarika jana siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake Machi 28 ambapo alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 39.

Afisa wa polisi jijini Atlanta, Andrew Smith ameongea na waandishi wa habari na kusema waliitikia wito baada ya kufahamishwa kuwa kuna sauti za mzozo na milio ya bunduki katika nyumba hiyo lakini milango ilikuwa imefungwa, wanaume wawili mmoja akiwa Scooter walikimbia kupitia mlango wa nyuma ya nyumba hiyo.

Afisa huyo anaendelea kusema walimpata Young Scooter nje ya uzio wa nyumba ya pili baada ya kuruka ambapo walimkutana majeraha ya mguuni ndipo walipomchukua na kumpeleka hospitali ya Grady Marcus ambako alifariki huko.

Hata hivyo, wakati wa mkutano huo wa wanahabari Smith alikanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zikisema kuwa Scooter aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi wa Atlanta.

"Ili tu kuweka wazi kabisa, jeraha ambalo lilipatikana kwa Scooter halikusababishwa na maafisa waliokuwepo eneo la tukio. Ilikuwa wakati mwanamume huyo alipokuwa akitoroka," amesema Smith.

Wasanii na watu maarufu wameomboleza kifo cha rapa huyo kupitia mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Playboi Carti, Quavo, na wengine wengi wakionesha kushitushwa na taarifa za kifo cha rapa huyo ambaye muda mchache alikuwa akifurahia siku yake ya kuzaliwa kupitia Insta Story yake.

Historia fupi ya rapa Scooter, alizaliwa huko South Carolina Machi 28, 1986. familia yake ilihamia Atlanta alipokuwa na umri wa miaka 9 , na kazi yake ya muziki imekuwa msingi tangu wakati huo.

Alianza kutamba kupitia wimbo wake wa 'Colombia' mwaka 2012 kabla ya kujiunga na wakali wa hip-hop Future, Juicy J na Young Thug kwenye ngoma ya 'DI$Function' mwaka 2014. Alitamba kwenye chati za Billboard kama msanii aliyeangaziwa kupitia ngoma ya 'Guwop' ya Young Thug, akishirikiana na Quavo & Offset kwenye 420 Hot kabla ya Migos kunjika.

Utakumbuka June 23, 2024 rapa Julio Foolio pia aliuawa kwa kupigwa risasi siku yake ya kuzaliwa ambapo alikuwa akisherehekea kutimiza miaka 26 kwenye moja ya appartment kuko Tampa, Florida nchini Marekani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags