Ally Kamwe akumbuka alivyopewa shavu na Tesa

Ally Kamwe akumbuka alivyopewa shavu na Tesa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema marehemu Grace Mapunda 'Tesa' ni kati ya watu waliomsaidia miaka saba iliyopita wakati akijitafuta.

Kamwe ameyasema hayo leo Novemba 4, 2024 wakati akizungumza kwa niaba ya Klabu ya Yanga, kwenye viwanja vya Leaders Club ambako ndiko shughuli za kuaga mwili wa Tesa zinafanyika.

"Ilikuwa mwaka 2017, nikiwa najitafuta, nilipenda sanaa ya maigizo, nilipenda kuandika nikatamani kuwa na kazi yangu, sikuwa na kipato. Nilimfuata Seleman Masenga akaniambia tutafute mwigizaji mkubwa, jina ambalo lilikuwa vichwani mwetu ni la Tesa ambaye alikuwa kwenye kiwango bora," amesema Kamwe.

Amesema licha ya kutokuwa na pesa, Tesa alimpa ushirikiano kwa kuifanya kazi.

Akizungumzia mfuko wa wasanii ambao Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alianza kwa kuchangia Sh15 milioni, Kamwe amesema Yanga chini ya Rais wake, Injinia Hersi itakabidhi Sh5 milioni kwenye mfuko huo.

Utakumbuka kuwa Tesa alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 2, 2024 kwa maradhi ya Nimonia, mwili wake unatarajia kuzikwa leo Novemba 4, katika Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags