Diddy asherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa Gerezani

Diddy asherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa Gerezani

Watoto saba wa mkali wa Hip Hop kutoka Marekani ambaye kwa sasa yupo gerezani kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono, jana Novemba 4, wamesheherekea siku ya kuzaliwa kwa baba yao kwa njia ya simu kutokea gerezani.

Watoto hao wameonekana wakiwa na furaha kufuatia video inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii huku wakiandaa keki na kumtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa kitendo ambacho kilimfurahisha huku katika ukurasa wake wa Instagram kukiwa kumechapishwa ujumbe usomekao kitendo hicho kimeifanya siku yake kuwa bora

Katika video hiyo Diddy pia alisikika akisema “Ninawapenda nyote, nawapenda sana, siwezi kusubiri kuwaona, najivunia nyinyi nyote, asanteni nyote kwa kuwa imara na kuwa upande wangu, nawapenda sana ninayo familia bora duniani” alisema Combs kwa njia ya simu

Sean John Combs ‘Diddy’ alizaliwa November 4, 1969 Harlem, New York, Marekani na kwa mara ya kwanza amesheherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa gerezani huku akisubiri kesi yake kuanza kusikilizwa Mei 5, 2025.

Combs alikamatwa kwa mara ya kwanza September 16, jijini New York kwa makosa kubwa unyanyasaji wa Ngono na mengineyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags