Uhusiano wa Mwana Fa na Mboni Mhita upo hivi

Uhusiano wa Mwana Fa na Mboni Mhita upo hivi

Ni miaka 23 sasa tangu Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' aachie wimbo wake 'Mabinti' wimbo uliobeba majina ya warembo maarufu waliotikisa kwa kipindi hicho.

Kati ya warembo waliotajwa kwenye wimbo huo ni Jay D, Ray C, Zay B na wengine. Hata hivyo lipo jina la Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita ambaye wakati anatajwa kwenye wimbo huo alikuwa bado binti mdogo. Utakumbuka alitajwa kama binti wa kigogo (tajiri).

Akizungumza katika mahojiano aliyofanya na Mwananchi, Mboni amesema wakati wimbo huo unatoka na jina lake kutajwa, alikuwa akisoma sekondari kidato cha pili.

"Mwana FA ni Mjomba wangu. Mdogo wa mama yangu. Wakati wimbo unatoka nilikuwa mdogo, nilikuwa Sekondari nadhani Form 2. Sisi kwenye familia yetu, We support each other. Na tuko very proud ya kila mmoja kwenye nyanja yake.

"Niliposikia nimetajwa nilikuwa sawa tu, na tulikuwa tunangoja video ya nyimbo. Nadhani aliwataja wale ambao kwenye mzunguko wake wa maisha walikuwa karibu nae. Wengi aliowataja naamini walikuwa watu anafahamiana nao. Mfano Mzuri ni Mimi,"amesema

Ameongezea kuwa ili mtu aweze kutimiza ndoto zake ni muhimu kujitambua, kujua uwezo wake na mapungufu yake. Ili kufahamu wapi pa kurekebisha .

"Jiamini na muhimu kuwa na uthubutu, usikubali kukatishwa Tamaa, na hata ikitokea una teleza, inuka. Inuka na uendelee,"amesema

Ikumbukwe kati ya mashairi yanayosikika kwenye wimbo huo wa FA ni haya,

"Yaani shwari hamna shari
Mi na mabinti damdam (kweli kweli)
Sababu zipo wazi mwenye macho aone enhh
Kuna kifua kama cha Zay B
Kiuno kama cha Ray C
Na pozi kama za Jay D
Sauti kama Fina
Au labda ya aunt Ndina ipo njema matabasamu
Kama binti Maumba wa kino Msio nidhamu

Mtafanywa mpende ngono Hold on!
Kuna pozi za kimtoni
Kama Tausi Likokola
Unataka ni full bakora
Mabinti wangara wanang'ara
Warefu warembo kama twiga
Mithili ya Happy Magese
Midomo kama ya Shose
Utapenda uonekane yaani viwanjani ututese
Au binti maarufu utasema Aina anatosha?
Kama nataka mwanya
Nafahamu wapi ntaupata
Mwite Aminata wa keita
Binti wa vigogo unamtafuta Mboni Mhita?,"ameimba Mwana FA kwenye wimbo wake huo uliotoka 2002 ukiwa ndani ya albamu yake iitwayo Mwanafalsafa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags