Ndaro ageukia kwenye muziki, ataja sababu

Ndaro ageukia kwenye muziki, ataja sababu

Masoud Kofii

Mchekeshaji maarufu nchini Masatu Ndaro 'Mjeshi Kikofia' ametangaza kuja na wimbo wake mpya utakao fahamika kama "Nimpe nini" aliowashirikisha G boy na Kontawa.

Ndaro ambaye wengi wamemfahamu kupitia sanaa ya vichekesho na maigizo kupitia jukwaa la Cheka Tu, linaloongozwa na Coy Mzungu ameimbia Mwananchi Scoop ameamua kuingia kwenye muziki kwa lengo la kusapoti vipaji na wasanii wengine na sio kwa lengo la kupata hela

"Nafanya muziki sio kwa sababu ya pesa kuna namna yangu ingine ya kupata pesa ambayo ni comedy mimi muziki nafanya kwa sababu ya kusapoti vipaji kama mwanangu G Boy ili afike anapostahili lakini pia kabla ya comedy nilikuwa nafanya muziki kwahiyo kuna muda nakaa idea zinakuja naamua kufanya"

"Napambana sana kumshika mkono G Boy naamini anakipaji kikubwa na Watanzania inabidi wamfahamu na ndiyo maana naweza kufanya wimbo nikampatia G boy kwa sababu ya kumsapoti"amesema

Amesema licha ya kutowekeza nguvu sana kwenye muziki lakini wasanii wengi wanakubali uwezo wake

"Mimi watu wengi ninaotembea nao na kuishi nao ni wanamuziki kwahiyo nikikaa nao wanaona kabisa ninakipaji hicho wengi wanaangalia matokeo watakayopata baada ya kufanya kazi na mimi na wanasifia sana,"amesema

Amesema anaamini katika kupambana hivyo siku moja anategemea kupokea Tuzo ya Muziki. Mpaka sasa Ndaro ana nyimbo zisizopungua tatu ambazo zimefanya vizuri tangu kuachiwa kwake zikiwemo "Nakwako Pia" aliomshirikisha Lady Mar, YouTube imetazamwa mara 176k,"Haupendwi" aliomshirikisha Gboy, YouTube 497k






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags