Usiku wa kuamkia leo Desemba 23,2024 imefanyika sherehe ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya msanii na mfanyabiashara Shilole ambaye aliambatanisha sherehe hiyo pamoja na kufurahia uwepo wa biashara yake ya chakula iliyodumu kwa miaka 10 hadi sasa.
Sherehe hiyo ilifanikiwa kuhudhuriwa na mastaa wa tasnia mbalimbali nchini akiwemo Diamond Platnumz, Zuchu, Lavalava, Mbosso na wengineo.
Hata hivyo katika sherehe hiyo mtoto wa pili wa Shilole anaye fahamika kama Rahma amesema anahofia kuwa kama mama yake.
"Mimi ninasomea Udaktari wa Chakula kwa Wamama na Watoto, mimi nahofia kuwa kama Shilole yeye ni msanii kwahiyo mimi sitamani kuwa kama yeye" alisema Ratima mtoto wa Shilole.
Rahma aliongezea kuwa mama yao hapendi wao waishi maisha ya mtandaoni na anataka wasome.
"Mama yetu alituambia elimu kwanza tukishamaliza ndio tutaanza kutumia mitandao ya kijamii," alisema Rahma.
Aidha Sherehe hiyo iliambatana na tukio Shilole kuvishwa pete na mpenzi wake mpya ambae alianza naye mahusiana baada ya ndoa yake na Rommy3D kuvunjika.
Ikiwa Shilole atafunga ndoa hii itakua ya tatu baada ya ndoa zake mbili za awali kuvunjika ambapo ndoa ya kwanza alifunga na Uchebe mwaka 2017 na ndoa yao ilivunjika mwaka 2020, ndoa ya pili alifunga na Romy3D 2021 na alitangaza kuvunjika kwake June 2024 takribani miezi sita iliyopita.
Leave a Reply