Mwaka unapinduka bila Video kutoka kwa Young Lunya

Mwaka unapinduka bila Video kutoka kwa Young Lunya

2024 ni mwaka ambao zimeachiwa albamu nyingi kutoka kwa wasanii wa Hip-hop nchini ikiwemo albamu ya Mbuzi kutoka kwa Young Lunya ambayo ilitoka rasmi June 28, 2024 ikiwa imeshiba ngoma 11.

Album hiyo ilifanya vizuri na inaendelea kufanya vizuri kwenye mitandao ya kuuzia muziki lakini licha ya kuwa na ngoma ambazo zinakubalika Mmaani bado Young Lunya hajaachia video wimbo wowote kutoka kwenye albamu hiyo, ikiwa ni karibu miezi sita sasa tangu albamu hiyo itoke.

Video za muziki kwa wasanii wa miaka hii inaongeza ufanisi zaidi kwenye kazi zao ni tofauti na wasanii wa zamani na mashabiki. Kwani walikuwa wanazingatia zaidi sauti na mashairi na ndio maana kuna nyimbo nyingi za zamani hazina video hadi leo lakini zinafanya vizuri.

Hilo ni tofauti kwa miaka ya sasa, msanii anahitaji kutoa video nyingi kulingana na audio hususani wasanii wanaoachia albama. Kutokana na video hizo kusaidia kwenye matangazo ya kazi hizo.

Hata hivyo baada ya Young Lunya kutoa albamu hiyo alipata nafasi ya kutumbuiza kwenye jukwaa la Nandy Festival Septemba 15, 2024 jijini Mwanza, ambapo ilikuwa show yake ya kwanza tangu kuachia albamu hiyo.

Katika shoo hiyo Mbuzi aliimba aliimba nyimbo zinazopatikana kwenye albamu tu, alipofanya mahojiano na Millard Ayo aliahidi kufanya ziara ya albamu hiyo pamoja na kutoa video mapema.

"Tour itakuja videos zitakuja kila kitu kipo kwahiyo tuendelee kusubiria," alisema Lunya

Album ya Mbuzi ina ngoma kama Natoka na Nani, Noma, Nduki, Mbwa Mwitu, She Is Mine Ft Jay Rox, Tungi, Toxic, Watoto wa Juzi Ft Sugu & Country Wizzy, Hatuna na Fame

Kumbuka Lunya ni mshindi wa tuzo za Tanzania Music Award TMA 2024 kwenye vipengele vya Msanii Bora wa Hip Hop wa mwaka na Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa Stupid aliomshirikisha Khaligraph Jones wa Kenya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags