D voice awachimba Mkwara wasabii wa Singeli

D voice awachimba Mkwara wasabii wa Singeli

Msanii wa WCB D Voice ametoa angalizo kwa wasanii wa singeli kutotoa nyimbo Desemba 31,2024 kwani watakula hasara.

“Wale Wasanii wa Singeli mnaosubiria mtoa nyimbo tarehe 31 mwisho wa mwaka. Msitoe maana video yetu ya 'Hujanizidi' ndio inatoka. Ni vyema mngetushabikia kulikoni hasara za bure. Ukilipata tangazo hili mwambie na mwenzio. Kwa ushauri tu lakini,” ameandika D Voice

Hujanizidi ni wimbo wa Zuchu aliomshirikisha Dvoice, unapatikana kwenye albumu yake mpya inayoenda kwa jina la Peace and Money iliyotoka Desemba 20,2024. Ikiwa na jumla ya Tracks 13 ambapo mpaka sasa ndio album namba 1 kwenye jukwaa la Audiomack nchini Tanzania.

Wawili hao wamekuwa na matokeo mazuri wanapokutana na kufanya kazi pamoja, utakumbuka ngoma ya 'Nani', 'BamBam', na 'Nimezama' zote zilifanya vizuri.

D Voice kabla ya kujiunga WCB alikuwa msanii aliyejikita zaidi kwenye muziki wa singeli na aina hiyo ya muziki ndiyo ilimtambulisha kwenye ulimwengu wa burudani, akitamba na ngoma kama Kuachana Shingapi, Mchanganyiko na zingine






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags