Denzel abatizwa, Atarajiwa kuwa Mchungaji

Denzel abatizwa, Atarajiwa kuwa Mchungaji

Mwigizaji wa Hollywood Denzel Washington amebatizwa rasmi Desemba 21, 2024 katika Kanisa la Kelly Temple of God in Christ lililopo kitongoji cha Harlem jijini New York, Marekani.

Wakati wa hafla hiyo ambayo ilikuwa mubashara kupitia ukurasa wa FaceBook wa kanisa hilo, Denzel alieleza safari ya maisha yake ya miaka 70 mpaka sasa ambapo ameamua kumpokea Mungu.

"Katika wiki hii moja ninatarajia kutimiza miaka 70, ilichukua muda lakini niko hapa ikiwa Mungu anaweza kunifanyia hivi hakuna kitu ambacho hawezi kufanya juu yangu," alisema Denzel baada ya kubatizwa

Mke wa mwigizaji huyo Pauletta ambaye pia alihudhulia ibada hiyo maalum akizungumzia furaha yake juu ya mafanikio ya kiroho ya mumewe alisema zaidi ya miaka 46 ya ndoa yao mpaka kufikia hapo ni Mungu tu

"Miaka arobaini na sita baadaye na bado nimesimama karibu naye hii yote imetokea kwani ni Mungu tu," alisema Pauletta mke wa Denzel

Hata hivyo baada ya sherehe hiyo Denzel alipiga picha akiwa ameshikilia cheti chake cha ubatizo na leseni ambayo itamruhusu kutawazwa na kuwa mchungaji siku zijazo kama atahitaji.

Hii inakuja baada ya nyota huyo wa filamu Novemba mwaka huu kueleza kuwa alifanya uharibifu mkubwa katika mwili wake kipindi alichokuwa akitumia dawa za kulevya na pombe kali kwa wingi huku akidai sasa ni mtu msafi na ameachana na matumizi ya vilevi kwa miaka 10 iliyopita.

Mbali na hayo mwigizaji huyo mwezi uliopita alitaangaza kustaafu kuigiza huku akiweka wazi kuwa Black Panther 3 itakuwa moja ya filamu zake za mwisho kucheza.

Pia kabla ya kustaafu kwake mwigizaji huyo amesema atafanya filamu nyingine kama Gladiator 2, na Othello.

Kwa miaka zaidi ya thelathini Denzel amekuwa na ushawishi mkubwa katika tasnia ya filamu, akifanya kazi kama mwigizaji, muongozaji, na mtayarishaji wa filamu huku akionesha umahiri wake waakucheza uhusika mbalimbali kuanzia uhusika wa kihistoria hadi wa kisasa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags