Waombolezaji wamuaga Tesa kwa picha

Waombolezaji wamuaga Tesa kwa picha

Mwili wa msanii, Grace Mapunda 'Tesa' umeagwa bila jeneza kufunguliwa. Kutoka na utaratibu uliowekwa na familia, ambayo ilitangaza kutofunua jeneza lenye mwili wa muigizaji huyo.

Awali kwenye viwanja hivyo familia iliwataka waombolezaji kutopiga picha na kusema atakayefanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.

Taarifa hiyo iliyotolewa na mdogo wa marehemu, Moses Mapunda, kwa kukazia kuwa jeneza lenye mwili wa Tesa halitafunguliwa na waombolezaji wataaga picha.

“Familia inawashukuru nyote kwa kutukimbilia katika msiba wa ndugu yetu, lakini imeamua jeneza la mpendwa wetu halitafunuliwa, mtaaga kwa picha,” amesema Moses Mapunda muda mfupi kabla ya waombolezaji kuaga jeneza lenye mwili wa Tesa.

Kutokana na taarifa hiyo, baadhi ya waombolezaji walianza kuondoka kabla ya zoezi la kutoa heshima za mwisho kuanza.

Utakumbuka kuwa Tesa alifariki dunia usiku wa kuamkia Novemba 2, 2024 kwa maradhi ya Nimonia, mwili wake unatarajia kuzikwa leo Novemba 4, katika Makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags