Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Edrisah Musuuza maarufu kama Eddy Kenzo ameteuliwa kuwania tuzo ya Grammy kitengo cha muziki bora unaochezwa dunia kote.
Kupitia shirika la habari la AFP mjini Kampala, Kenzo ameeleza kuwa, "Uteuzi huu unafaa kuwapatia matumaini wasio na uwezo. Siwezi kuelezea hisia zangu ni kama ninaota.”
Msanii huyo aliyeimba kibao kilichotamba Afrika Mashariki na nje yake ‘’Sitya Loss" (siogopi Hasara) anasema , "Uteuzi huu unafaa kuwapatia matumaini wasio na uwezo," anasema Bw Kenzo "Hata masikini zaidi na wenye maisha ya chini sana wanaweza kama nimeweza, na wao wanaweza pia ."aliongeza.
Kwa miaka mingi Kenzo ameweza kushinda tuzo kadhaa kutokana na muziki wake uliochanganywa mtindo wa dancehall na Afrobeat, ikiwa ni pamoja na Tuzo za Nickelodeon Kids' Choice mwaka 2018, BET mwaka 2015, na tuzo nyingine nyingi za All Africa Music .
Na sasa huenda akapeleka nyumbani tuzo ya Grammy kwa kibao chake cha "Gimme Love", wimbo wake wa mwaka 2022 ulioimbwa kwa Lugha za Luganda, Kiingereza akishirikiana na mwanamuziki wa Marekani Matt B.
Tuzo hizo zinazotarajiwa kutangaza mshindi wakati washindi tarehe 5 Februari ambapo anakabiliana dhidi ya nyota wa Afropop Mnigeria Burna Boy miongoni mwa wanamuziki wengine wanaowania tuzo hiyo.
Leave a Reply