Biashara ya utengenezaji na upakaji wa rangi kwenye kucha

Biashara ya utengenezaji na upakaji wa rangi kwenye kucha

Niaje watu wangu wa nguvu! It’s another Friday kwenye chimbo letu la biashara tukitoa nondo zinazohusiana na biashara ikiwa pamoja na faida na changamoto za biashara hizo.

TAZAMA VIDEO HAPA

Basi bhana leo nakukaribisha kuijua biashara ya utengenezaji na upakaji wa rangi kwenye kucha ambayo unaweza kuianza ukiwa na mtaji mdogo. Twende pamoja kuijua biashara hii kiundani zaidi.

NAMNA YA KUANZISHA BIASHARA HII

  • Mtu anayetaka kuanza biashara hii anatakiwa awe na nia ya dhati na kuipenda biashara hiyo.
  • Anatakiwa kujua eneo atakalofungua ofisi kwa ajili ya biashara hiyo.
  • Anatakiwa kujua aina ya wateja wake ili aweze kuweka ubunifu au kukabiliana nao ,mfano gharama ya upakaji wa rangi kwenye kucha, rangi gani pendwa nk
  • Anatakiwa awe na lugha nzuri kwa wateja wake pia kujua kwa uchache elimu ya biashara.

MTAJI NA VIFAA VYA KUANZA BIASHARA HII

Mtaji wa kuanza biashara hii unategemea na mfanyabiashara mwenyewe namna atakavyoitengeneza ofisi yake kwa mapambo anayoyapenda, lakini kwa mtu anayeanza biashara hii bila kuweka mambo mengi anaweza kuanza na mtaji wa Tsh80,000/= pamoja na vifaa vifuatavyo;

  • Msasa wa miguu 1pc Tsh1000/=
  • Nail cutter 1pc Tsh5000/=
  • Gundi Tsh2500/=
  • Kucha 1 dozen Tsh7000/=
  • Remover 1litre Tsh12,000/=
  • Sabuni 1 litre Tsh3000/=
  • Mashine inaanzia Tsh30000/= na kuendelea kulingana na uhitaji wako.
  • Ndi fail 1 Tsh1000/=
  • Rangi za kucha 1 dozen Tsh18,000/=
  • Taulo1 Tsh2000/= ila unaweza kuongeza kulingana na matakwa yako 

Hivyo ndo vifaa vinavyotumika kuianza biashara ya utengenezaji na upakaji wa rangi kwenye kucha ambayo ni biashara inayokuwa kwa kasi sana kila kona ya jiji la Dar es salaam.

CHANGAMOTO KATIKA BIASHARA YA UTENGENEZAJI NA UPAKAJI WA RANGI KWENYE KUCHA

Kama inavyofahamika kila biashara haikosi changamoto tena kwa biashara kama hii ambayo soko lake kuu ni wadada, baadhi ya wafanyabiashara wamezungumza changamoto wanazokutana nazo katika biashara hiyo ikiwemo pamoja na;

  • Wateja kuwa wasumbufu wakati wa utengenezaji wa kucha. Mteja anapokuja kupaka rangi au kutengeneza kucha, mtengenezaji kulingana na aina yake ya vidole au kucha anelewa namna gani ya kutengeneza kucha katika shape tofauti tofauti kama shepu ya box, mdomo wa kuku pia aina ya rangi itakayompendeza kulingana na rangi yake, lakini changamoto inakuja pale mteja anaona uanavyopakwa rangi, akimaliza anasema rangi hajaipenda so unaifuta na kumpaka nyingine ambapo hasara inakuwa kwa mtengenezaji kwenye vifaa na pia muda.
  • Wateja kuwa na mazoea. Wateja wengine wanachukulia kujuana kuharibu biashara ya mtu na kama inavyofahamika soko lenyewe ni wanawake, lazima umkarimu ili kesho arudi tena au kukuletea wateja wengine. Hii inakuwa changamoto kwani wengine wanakuwa hawalipii huduma kutokana na mazoea, heshima na uaminifu mliowekeana.
  • Ushindani kuwa mkubwa. Hii pia ni changamoto ambapo inawafanya wafanye kazi nje ya maadili ya kazi yao ili kuwavutia wateja kwa huduma nzuri, mfano kuosha miguu au kuwamassage miguu sio kitu kizuri ila inawabidi wafanye hivyo kama mbinu ya kuvutia wateja na kufanya watengeneza kucha waonekane wahuni.
  • Mteja kutovaa nguo nzuri anapokuja kupata huduma hii,kwa mfano mtu kuvaa sketi fupi hii inawasababishia matamanio.

Aloooh! Kweli siri ya mtungi aijuaye kata. Wafanyabiashara hawa wanakutana na changamoto nyingi kutoka kwa wateja wao ila mtaani tunawalaumu wao bila kujali upande wa pili ambao ni wateja wao. Kazi yangu kukusogezea fursa za biashara kazi kwako kufanya uamuzi.

Until next week, bye bye!






Comments 1


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post