Wataalamu kutoka Ufaransa kuja kufanya uchunguzi ajali ya Precision Air

Wataalamu kutoka Ufaransa kuja kufanya uchunguzi ajali ya Precision Air

Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania umesema kikosi cha wataalamu kadhaa kutoka Kituo cha Ufaransa cha uchunguzi na uchambuzi wa masuala ya usalama wa ndege kilitarajiwa kuwasili nchini Tanzania jana ili kusaidia kufanya uchunguzi wa ajali ya Precision Air iliyotokea Bukoba, Kagera.

Taarifa ya Ubalozi huo kwa vyombo vya habari imesema, “Ndege hiyo iliundwa na makampuni mawili makubwa ya anga ya Ulaya ambayo ni AIRBUS na LEONARDO.”

“Kikosi hicho cha wataalamu kitasaidia katika uchunguzi kwa lengo la kugundua hatari zilizosababisha kutokea kwa ajali hiyo,” imeeleza taarifa hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post