Mambo vipi watu wangu wa nguvu mwezi Machi umekuwa wa kipekee, swaumu zimetaradadi kila kona, bila kuwachosha mwezi huu mzima nitakusogezea tips mbalimbali za chakula, ambazo zitakusaidia katika mfungo wako. Na hata kama siyo wewe basi unaweza kufanya biashara ya vyakula vya aina hii.
Katika kipindi hichi biashara ambayo watu wengi hufanya ni yakuuza futari jioni, ni moja ya biashara ambayo ukituliza akili basi utaiona faida yake, sasa wachakarikaji wenzangu nataka kuwapa tips za vyakula ambavyo mnatakiwa kupika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kama tunavyojua ukiwa katika swaumu mwezi mzima lazima kuna baadhi ya vitamin vinaweza kupotea mwilini mwako, hivyo basi wapishi wa futari hasa wafanyabiashara wanatakiwa kuzingatia mlo sahihi wakati wa kufungulia (kufuturu) ili kuendelea kuimarisha afya za walaji.
Mara nyingi vyakula vinavyoliwa kwa wakati huu ni aina ya mizizi kama vile mihongo, magimbi, viazi vitamu, vyakula ambavyo vyote vipo katika kundi la mlo mmoja, jambo ambalo halishauriwi kiafya.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) vipo vyakula vinavyofaa na visivyofaa kuliwa wakati wa kufungulia katika msimu huu wa Ramadhan ikiwemo vyakula vyenye chumvi nyingi hivi havifai kwani vinaleta kiu na mwisho ukashindwa kufunga siku inayofuata.
Aina vya vyakula vinavyoshauriwa kuliwa/ kupikwa wakati wa kufungulia
Wakati wa kufungulia hutakiwi kula vyakula vizito kwani vinaweza kukusababibisha kuumwa na tumbo kutoka na kutokula chochote tangu asubuhi. Hivyo basi wafanyabiashara wa futari wanatakiwa kuacha kupika vyakula kwa mazoea kuwa futari lazima mihogo au magimbi.
Kinyume chake vipo vyakula vyepesi ambavyo vinafaa kuliwa na mfungaji ni vile vyepesi vikiwemo supu, mtori, mchemsho wa ndizi, na vingine ambavyo vya kawaida ikiwemo tambi, chapati za maji na viazi rosti kwa upande wa vinywaji uji, chai pamoja na maziwa.
Ujumbe kwa mlaji
Inashauriwa kula hivyo kutokana na kusaidia mmeng’enyeko mzuri wa chakula.
Aidha ulaji wa tenge kama kianzio ni vizuri kwa kuwa inamsaidia mfungaji kupata nguvu kwani mtu anapofunga hupoteza nguvu hivyo basi ulaji wa tende kama kianzio husaidia kupata nguvu kwa wingi.
Zingatia haya;
Ni wazi kwamba kipindi cha mfungo wa Ramadhani kama hiki, siyo tu suala la chakula utakachokula, lakini pia kiwango cha chakula na aina ya chakula unachokula, kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha mwili unakuwa na afya njema kila wakati.
Ili kuwa na nguvu na virutubisho vinavyohitajika mwilini kila siku, unatakiwa kula vyakula vyenye protini, wanga, vitamini na madini mengine, pia unatakiwa kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha.
Leave a Reply