Idris Sultan awafunda vijana

Idris Sultan awafunda vijana

Mwigizaji na mshindi wa Big Brother Afrika 2014, Idris Sultan amewataka vijana kupunguza kutembea na makaratasi badala yake wajitambue kuanzia kichwani.

Idris ameyasema hayo huku akitaka watu kubadilika kutumia CV za kuandika na badala yake kuwa nazo kichwani ili iwasaidie pindi wanapokutana na watu wenye fursa ambao wanapenda kusikiliza zaidi na siyo kusoma CV.

"Naombeni niwafundishe jinsi ya kuwa na CV kichwani muachane na makaratasi, jinsi mabilionea wanafanya kazi, kitu wanajali ni muda wake ukikaa lazima ajue kwa nini akusikilize wewe. Ilikupata hiyo lazima CV yako iwe kichwani kwa hiyo ukikutana na mtu unamwambia mfano. Samahani fulani mimi ni Idris Sultan mwigizaji, movie yangu ya kwanza imesumbua sana Netflix na mshindi wa Big Brother 2014, kuna kitu nilikuwa nafikiria unaweza nisaidia na nikakusaidia pia na wewe," amesema Idris Sultan

Pia Idris ameendelea kwa kuzungumzia namna ambavyo matajiri na ma-boss walivyo wagumu kusoma CV zilizoandikwa na hiyo sio kwa sababu ya dharau bali mambo mengi waliyonayo.

"Matajiri wanatunza sana muda unahisi tajiri anavyojali muda anaweza kuanza kusoma vitu anatafuta nini wanahitaji kuambiwa ili wajue tuwe na mbio tunapoona nafasi ya kutoka,"amesema.

Idris Sultan amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 12, katika mkutano kwa ajili uzinduzi wa tamasha la Global Entrepreneurship Festival (GEF) linalotarajiwa kufanyika kati ya Novemba 22 hadi Novemba 24, 2024 huko Akure nchini Nigeria.

Tamasha hilo limelenga kuwakutanisha wajasiriamali maarufu, viongozi mashuhuri na wabunifu kutoka nchi mbalimbali duniani, likiwa na lengo la kuhamasisha ukuaji wa biashara na kubadilishana maarifa.
Hata hivyo, tamasha hilo litaenda sambamba na ugawaji wa tuzo kwa watu mbalimbali kunzia wajasiliamali na viongozi wa taasisi zinazotoa mchango kwenye jamii zao. Tuzo hizo zitakuwa katika vipengele 16 ambavyo vitashindaniwa na watu 40






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags