Viatu vitavyoongeza muonekano wa vazi lako

Viatu vitavyoongeza muonekano wa vazi lako

Na Asha Charles

Kawaida fashion hubebwa na muoneano, kuanzia juu mpaka chini yaani mavazi, nywele, viatu na hata harufu ya muhusika. Wapo ambao hujikuta wakiharibu muonekano wao kwa kupuuzia kitu kimoja. Kwa mfano unaweza kupendeza lakini miguuni viatu vikakuangusha.

Kutokana na hilo Mwananchi Scoop imekuletea viatu vitakavyoongeza muonekano wako. Kwanza kabisa kuna mitindo na rangi zisizo chuja au kupitwa na wakati katika viatu, mwongozo huu utakufundisha jinsi ya kuchagua viatu vya kuvaa na vazi bila kujali rangi, tukio au msimu.

 

      Chagua rangi za viatu zinazofanana na nguo zako

Hapa unaweza kuvaa viatu vyovyote unavyopenda na vinavyoendana na nguo yako ilimradi hakuna kanuni ya mavazi. Mfano ukivaa kiatua cheusi ni rahisi kwa kuvalia mtindo wowote wa mavazi au rangi yoyote.  

      Kwa mavazi ya kawaida vaa viatu vinavyong’aa

Ongeza aina ya viatu vya rangi kwa kulinganisha mavazi yako yaliyo na rangi za kupoa itakuletea muonekano mzuri, hapa sasa utajaribu kiatu chenye muundo mzuri mfano kiatu cha ngozi, ikiwa umevaa blauzi nyepesi au ya mterezo na suruali fupi ya jeans.

 

      Epuka kumechisha rangi

Usivae rangi moja kuanzia juu hadi chini, ikiwa una blauzi ya blue na skirt ya blue, epuka kuvaa viatu vya rangi hiyo hautapata muonekano wenye kupendeza.

Hapa watu wengi huwa wanafeli kwa ‘kumechi’ full kama askali kanzu wa enzi za mkoloni, kwa mantiki hiyo huwezi kuwa wa kuvutia machoni kwa watu na utaonekana wa ajabu.

 

      Chagua rangi za kawaida

Hapa usitake makuu sana kwa sababu katika mitindo kuna hitaji mpangilio hivyo chagua rangi za kawaida za viatu ambazo zitakufanya uwe na muonekano nadhifu.

 

Hakuna kitu kizuri kama kujihisi hali ya kujiamini pale unapopangilia mavazi yako hadi kiatu, hapo kama unaenda kwenye sherehe unakuwa na muonekano wa kipeke na kama unavyojua mwanamke akipendeza kuanzia juu hadi chini huwa anajijua bhana.

 

      Chagua viatu sahihi kwa msimu

Unaweza kuchagua viatu vya msimu wa baridi na viatu vya kiangazi kadiri nguo zako zinavyobadilika.

Kama majira ya joto ni wakati wa kufurahia viatu vyako vya espadrilles (viatu vya nguo) viatu vya aina hiyo ukivaa vinapitisha hewa na vinafanya miguu yako kutodhoofika kwa ajili ya joto.

Kwa majira ya baridi chagua loafers (kiatu cha ngozi), hakikisha kwamba kisigino chake ni kipana ili kuepusha kuteleza wakati wa mvua.

Bado unaweza kunyumbulika hata kwa majira ya baridi, lakini epuka viatu na espadrilles kwa sababu havifanani na vitambaa vizito na rangi ya vuli.

 

      Viatu vyenye visigino virefu

Nguo ambazo tayari husaidia kurefusha mguu wako, kama vile sketi za penseli na suruali nyembamba Stiletto hujenga udanganyifu wa urefu zaidi, na kufanya miguu yako iwe myembamba zaidi na yenye kuvutia.

 

Hasa kwa watu wenye vimo vifupi viatu vya kisigino virefu vinapendeza na kufanya nguo kuonekana vizuri.

Mara nyingi viatu vinavyovaliwa na sketi ndefu vinaweza kumfanya mwanamke aonekane mchafu kama hatozingatia aina ya viatu ambavyo anatakiwa avae kutokana na mtindo wa sketi yake.

      Vaa viatu vya riadha vilivyoundwa kwa ajili ya mchezo

Ikiwa wewe ni mkimbiaji, mwanamichezo au unafanya mazoezi unatakiwa uvae viatu husika vya michezo, kwa mfano vya kukimbia vya insoles (kiatu cha mazoezi).

Huwezi ukavaa buti za kawaida kwa ajili ya michezo kwa sababu kuna viatu ambavyo haviwezi kuhimili mikiki kama insoles hivi vinakuwa special kwa ajili ya kukusadia kufanya mazoezi ukiwa cormfortable.

 

Kwa mantiki hiyo itoshe kusema kwamba fashion ni maisha ya kila siku mwanetu sisi kama Team Mwananchi Scoop tunalithibitisha hilo na ndiyo maana tunakujuza mapya kila weekend. Tukutane next week kwa ajili ya mambo mapya katika fashion.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post