Ariana Grande na Beyonce wanavyokiwasha katika filamu za muziki

Ariana Grande na Beyonce wanavyokiwasha katika filamu za muziki

Na Asma Hamis

Licha ya kukimbiza kwenye muziki wasanii kutoka Marekani Ariana Grande na Beyoncé Sasa wanatajwa kuonesha uwezo wao kwenye filamu za muziki.

Kwa mujibu wa tovuti ya billboard anaeleza kuwa Ariana Grande ataonekana katika filamu ya Wicked inayotarajiwa kutoka Novemba 22, mwaka huu huku akishirikiana na mastaa kama Cynthia Erivo, Jonathan Bailey, Ethan Slater, Michelle Yeoh na wengineo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ariana kushiriki katika filamu kwani amewahi kuonekana katika filamu kama Swindle ya mwaka 2013 akiigiza kama Amanda, Don’t Look Up ya mwaka 2021 akiigiza kama Riley Bina, Hairspray live ya mwaka 2016 akiwa kama Penny Pingleton na nyinginezo.

Ariana sio msanii pekee kutoka Marekani kufanya filamu kama hizo yupo Beyoncé ambaye naye anakimbiza zaidi katika filamu za muziki ambapo amewahi kuonekana kwenye filamu kama Dreamgirls ya mwaka 2006 alicheza kama Deena Jones, nyingine ikiwa yam waka 2009 iitwayo Obsessed akicheza kama Sharon Charles akishirikiana na muigizaji maarufu Idris Elba.

Licha ya wasanii hao kuzitendea haki filamu za muziki lakini pia wapo wasanii wengine akiwemo Madonna kupitia filamu ya Evita yam waka 1996 akicheza kama Evita Peron, huku juhudi zake zikizaa matunda na kumpatia tuzo ya Mwimbaji Bora wa Vichekesho (Golden Globe).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags