Rais Samia atuma salamu za pole kifo cha King Kikii

Rais Samia atuma salamu za pole kifo cha King Kikii

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kutokana na kifo cha nguli wa muziki wa dansi Tanzania, Boniface Kikumbi maarufu King Kikii.

Salamu hizo amezitoa kupitia mitandao yake ya kijamii leo Ijumaa Novemba 15, 2024.

“Ninatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wasanii na wapenzi wote wa muziki nchini kufuatia kifo cha mwanamuziki nguli Boniface Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’.

“Kwa zaidi ya miaka 50 King Kikii ametoa burudani kwa mamilioni ya Watanzania na amekuwa mlezi na mwalimu wa wengi katika tasnia ya muziki. Tutamkumbuka na kumuenzi kwa kazi zake nyingi na nzuri ikiwemo wimbo wake maarufu wa ‘Kitambaa Cheupe’ ambao umeendelea kuwa sehemu ya burudani kwenye maeneo na shughuli mbalimbali za burudani nchini,” ameandika Rais Samia

King Kiki amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77, usiku wa kuamkia leo huku familia ikikitaja chanzo kuwa ni saratani ya ini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags