King Kikii wa Kitambaa cheupe afariki dunia

King Kikii wa Kitambaa cheupe afariki dunia

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Tanzania, Boniface Kikumbi maarufu King Kikii amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 15, 2024 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Taarifa za kifo cha King Kikii zimethibitishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa asubuhi ya leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Lala salama mzee wetu Boniface Kikumbi Mwanza Mpango (King Kikii), mwanamuziki mkongwe, jabali la rhumba na mtu mwenye utumishi uliotukuka katika tasnia ya muziki Tanzania.

“Tutauenzi mchango wako mkubwa katika muziki wa dansi Tanzania. Kwa miaka mingi umeburudisha, umefundisha, umeelimisha na uliipenda sana Tanzania,” ameandika Msigwa.

Enzi za uhai wake, King Kikiii alitamba na vibao mbalimbali kikiwemo maarufu cha ‘Kitambaa cheupe’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags