Jumatatu Machi 24, 2025, Jaji J. Paul Oetken alitupilia mbali mashtaka yaliyofunguliwa na mtayarishaji muziki 'Rodney Lil Rod Jones' dhidi ya 'Diddy Combs' .
Ni mashtaka yaliyofunguliwa na Jones akidai wakati anafanya kazi ya kuandaa albamu ya Diddy inayoenda kama The Love Album: Off the Grid, alishuhudia na kuhusishwa kwenye mambo machafu yasiyofaa. Jones alidai aliishi na Diddy wakati alipokuwa akitayarisha albamu hiyo kati ya Septemba 2022 na Novemba 2023.
Katika kipindi hicho, anadai alikuwa shahidi wakati Diddy akitumia madawa ya kulevya aina ya kokeini kuwalewesha na kufanya ngono na wasichana wadogo mbele yake. Kusafirisha wanaume na wanawake kwa biashara ya ngono pia alidai hakulipwa fidia ya kutosha kutokana na mchango wake kama mtayarishaji wa album hiyo.
Hata hivyo kutokana na madai hayo jaji huyo wa Wilaya ya Marekani J. Paul aliamua kufuta kesi hiyo kutokaa na Jones kushindwa kutoa ushahidi wa kutosha katika kuunga mkono madai yake.
Hivyo hakimu alisema hakuna uhusiano wa wazi kati ya madai ya shughuli haramu na kushindwa kumlipa Jones kwa kazi yake aliyofanya kutayarisha album ya The Love Album: Off the Grid.
Lakini pia, madai mengine yaliyotupiliwa mbali dhidi ya Diddy, ni pamoja na yale yanayohusiana na ufisadi (RICO) na mengine ni ya kihisia, na yale ya uvunjaji wa mikataba.
Mahakama imeruhusu kuendelea kwa madai mengine dhidi ya Diddy hasa yale yanayohusu unyanyasaji wa kijinsia na kingono.
Kesi hii ni sehemu ya mfululizo wa changamoto za kisheria ambazo Diddy amekumbana nazo tangu mwanzoni mwa 2024, zikiwemo tuhuma za unyanyasaji wa kingono na vitendo vingine haramu.
Utakumbuka Diddy mara kwa mara amekuwa akikanusha madai yote yanayomkabili ambapo kwa sasa anakabiliwa na mashtaka mengi ya unyanyasaji wa kijinsia na mashtaka ya biashara ya ngono huku kesi yake ikipangwa kusikilizwa tena mwezi Mei 2025

Leave a Reply