Zijue nguo ambazo mwanamke mwenye matiti makubwa hatakiwi kuvaa

Zijue nguo ambazo mwanamke mwenye matiti makubwa hatakiwi kuvaa

Hellow!! Once again on Fashion tumekutana tena hapa katika jarida lako pendwa la Mwananchi Scoop ilikupeana updates mbalimbali katika Fashion, nikusihii tu twendelee na weekend yetu ukiwa na kitu kipya kwenye ulimwengu wa mitindo.

Leo katika section yetu ya Fashion tutajuzana aina za nguo ambazo huwatakiwi kuvaa wanawake au mwanamke mwenye matiti makubwa.

Kwanza kabisa wewe mwanamke mwenye matiti makubwa unatakiwa ujikubali jinsi ulivyo maana ni maumbile yako uliyo jaaliwa, japo kuna baadhi ya wanawake huwa hawajikubali na kuchukia kuwa na matiti makubwa labda ni kwambie tu siri ya urembo wa mwanamke kwanza ni kujikubali jinsi ulivyo, halafu unaanza kujitafuta katika mtindo kipi ambacho kitakufaa katika mwili wako hasa katika mavazi unatakiwa kufahamu ni mavazi gani yataendana na mwili wako.

Wewe mdada mwenye matiti makubwa kwanza unatakiwa utafute ‘brazia’ ambayo itatosheleza matiti yako kabla ya yote ili ukivaa nguo iweze kukukaa vizuri, epuka kuvaa brazia za ‘sponji’ zitafanya matiti yako kuwa makubwa zaidi.

*Epuka kuvaa nguo za mpira na zenye kubana sana mara kwa mara maana zitachoresha matiti yako nakufanya kuwa na muonekano mbaya, unashauriwa kuvaa nguo ambazo zina nafasi ili ipunguze muonekano wa matiti kuwa makubwa.

*Epuka kuvaa nguo za wazi ambazo zitaonesha mgongo wako na kuacha ‘brazia’ yako ionekane utapoteza urembo wako maana kwa vyovyote matiti yatachukua nafasi yake.

*Epuka kuvaa kunguo za wazi kwa sababu sehemu kubwa ya kifua chako imebebwa na matiti hivyo si busara kuvaa nguo za wazi na haitakufanya kuwa na muonekano mzuri badala yake utakuwa kituko kila unapopita.

*Epuka kuvaa ‘brauzi’ fupi hazitakupa muoneakano mzuri kifuani kwako kutokana ukubwa wa matiti, hakikisha una vaa ‘brauzi’ inayotosheleza katika mwili wako na usijilinganishe na wanawake wenye matiti madogo.

*Epuka kuvaa nguo zenye kambakamba kama fashion maana hazitakupa muonekano mzuri kutokana na ukubwa wa matiti yako.

Mwanachi Scoop iliweza kupata ushuhuda wa mwanamke mmoja aitwaye Amina Muhidini mkazi wa Charambe, Dar es salaam ambaye katika mtaa wake baadhi ya watu walikuwa wakimtania kutokana na matiti yake kuwa makubwa.

Yeye anatueleza kuwa mwanzo wakati anaanza kukua aliona ajabu matiti yake kuongezeka kuliko wanawake wengine na ilikuwa ikimtesa hali hiyo.

Hii inaweza ikakushangaza kwa sababu kuna watu wanaenda kufanya hadi upasuaji ili kupata matiti makubwa lakini kwake ilikuwa tofauti na ilimchukua muda mrefu kukubaliana na hali hiyo anasema.

“mwanzo nilikuwa nikiona kama mzigo kwa sababu nilikuwa sijui jinsi gani ya kuyaweka matiti yangu, hiyo hali ilinitesa lakini sasa najikubali kuliko mwanzo na ninapenda ninavyovaa na wala yale majina ya ajabu niliokuwa naitwa mtaani sasa hivi hakuna tena”

Amina aliwataka wanawake wenye matiti makubwa wajikubali na kuvaa nguo ambazo zinawafaa kutokana na maumbile yao.

Naweza kukwambia tu kujikubali ndiyo jambo la msingi hasa katika urembo na kuachana na mambo ya kuiga vitu ambavyo haviendani na wewe hasa katika mavazi.

 Naye mwanamitindo wa zamani Bi Tahya Peter mkazi wa Dar es Salaam aliweza kutoa maoni yake akieleza kuwa siku hizi mambo yamebadilika wanawake wamebadilisha urembo na kuwa kituko,  zama hizi yaani asiyekuwa na matiti makubwa anahitaji kuongeza na mwenye nayo anatamani kuyapunguza kwa maana yake tofauti na zamani anasema.

“Enzi zetu sisi ilikuwa ukimkuta mwanamke kwanza matiti yake yapo wazi lazima watu wamshangae sana, sasa imekuwa tofauti, unaweza ukamuona mwanamke ana maumbile makubwa ya matiti yake anavaa nguo za wazi bila kuogopa kisa amewaona wanawake wa ughaibuni (nchi za nje) anajisahau kuwa yeye ni mwanamke wa kiafrika kuwa hatuna mila hizo.

Unakuta hata hapendezi kuvaa hivyo ila kwa sababu amevaa mtu maarufu kutoka nje basi na yeye anaiga bila kutazama maumbile yake.”

Bi Tahya ameeleza wao zamani walikuwa wakishona nguo zinazoendana na maumbile yao.

“zamani tulikuwa tukishona nguo nzuri za kusitiri haya matiti yetu yasionekane hovyo, nguo zinazoziba kifua chote ilikuwangumu kuona matiti ya binti, ila hivi sasa mambo yamekuwa tofauti kutona na utandawazi na sidhani kama wanawake wakisasa watabadilisha maono yao juu Fashion za kuiga kutoka mataifa ya mbali.”

Aliwataka mabinti kurudi kama ilivyo awali na wajikubali mionekano yao na kuacha tabia ya kuiga sana fashion za kutoka nje maana zinaweza kuharibu vizazi vijavyo katika mitindo ya uvaaji.

Mimi huwa nakwambia katika jarida lako la Mwananchi Scoop huwa tunaenda mbali zaidi kuhusu Fashion I hope utakuwa umeondoka na kitu na umejua chakufanya kuhusiana na mada hii ya leo naamini ilikuwa kati ya somo zuri la fashion, tukutane tena next weekend maana kuna mengi mazuri!!!.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post